Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Anywesha watoto sumu kwa wivu wa mapenzi
Habari Mchanganyiko

Anywesha watoto sumu kwa wivu wa mapenzi

Spread the love

SELEMANI Mashaka Haruna (31), Mkazi wa Majengo wilayani Urambo, Tabora anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuuwa mtoto wake kwa sumu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

Akizungumza kuhusu tukio hilo leo tarehe 30 Aprili 2019, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Emmanuel Nley amesema, tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana.

Kamanda Nley amesema, Haruna anadaiwa kuwapa watoto wake wa kufikia soda yenye sumu, ambapo mmoja aliyefahamika kwa jina la Nyamizi Ally (7) amefariki huku Kalunde Ally (4) akidhurika.

Kamanda Nley amesema, uchunguzi wa awali umebaini kwamba, chanzo cha mtuhumiwa huyo kuwanywesha sumu watoto wake wa kufikia ni wivu kwa kuwa, alikua hataki kuishi na watoto hao.

“Tarehe 29 Aprili 2019 majira ya mchana Jeshi la Polisi tulipata taarifa ya tukio hilo, tulifika kwa mtuhumiwa na kumkamata . Uchunguzi wa awali unaonesha alikuwa na chuki na watoto wake wa kufikia, alitaka waende kwa baba yao,” amesema Kamanda Nley.

Kamanda Nley amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na kwamba ukikamilika hatua zaidi za kisheria zitachukukiwa dhidi ya mhusika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

error: Content is protected !!