April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tisa wadakwa kwa kuiba mafuta ya Transfoma

Spread the love

JESHI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata watu tisa kwa tuhuma za wizi wa mafuta ya transfoma na vifaa vyake. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 30 Aprili 2019 jijini Dar es Salaam, kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa, walisema mafuta ya transfoma huyauzaa kwa Praygod Kimaro na Selemani Baraka.

Amesema, polisi walifika katika stoo ya Praygod na duka la Seleman watu ambao wanatuhumiwa kuuziwa mafuta ya transfoma na watuhumiwa hao, na kufanikiwa kukamata madumu 68 ya lita 20 ya kampuni za mafuta za Total, Cat, Fuchs na BP.

“Tarehe 25/7/2019 majira ya saa tano usiku, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), liliendesha oparesheni ya kuwasaka watu wanaohujumu miundombinu ya TANESCO katika maeneo mbalimbali ya Jiji la DSM.

“Lilifanikiwa kumkamata Shukuru Hamisi (39), Mkazi wa Tabata akiwa katika ghala la TANESCO lililopo Kigamboni, akiiba mafuta ya kwenye transfoma yenye namba T.26840 aina ya TCO ya mwaka 2007,” amesema Kamanda Mambosasa.

Amesema, baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo, aliwataja wenzake anaoshirikiana nao ambao ni Mahmoud Ramadhan (39) Mkazi wa Tabata, Witnes Elimasia (35) Mkazi wa Kimara, Japhet Senyagwa (34) mkazi wa Kinyerezi, Yusuph Salum (38) mkazi wa Mbande Chamazi, Shabani Juma (42) mkazi Tabata Kifuru na Richard Adam.

“Jeshi la Polisi, Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na maofisa wa TANESCO, walifika katika stoo ya Praygod Kimaro na duka la Selemani yaliyoko Tabata dampo na kufanikiwa kukamata madumu 68 ya lita 20  ya makampuni ya mafuta ya TOTAL, CAT, FUCHS, PERFOMAX, CASTROL OIL, BP, MOGAS, LUBEX.

“Pia lilikamata maboksi 127 yenye nembo za kampuni hizo, machujio mawili ya mafuta, kitabu chenye oda mbalimbali za wateja wake wa mafuta na mapipa mawili yenye ujazo wa lita 200 yakiwa na mafuta ya transfoma,” amesema Kamanda Mambosasa.

Amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka Praygod Kimaro, Selemani Mrutu na watuhumiwa wote waliokamatwa, watafikishwa mahakamani hivi karibuni.

error: Content is protected !!