Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Tulia ampa maagizo Prof. Mkumbo
Habari za SiasaTangulizi

Spika Tulia ampa maagizo Prof. Mkumbo

Prof. Mkumbo
Spread the love

SPIKA wa Bunge, Dk.Tulia Ackson, amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, kufanya tathimini ili kujua wilaya zinazohitaji vituo vya mabasi ili Serikali ielekeze nguvu kujenga katika maeneo yenye uhitaji mkubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Spika Tulia ametoa agizo hilo, baada ya wabunge, Joseph Tadayo (Mwanga), Ezra Chiwelesa (Biharamulo) na Victor Kawawa (Namtumbo), kuhoji lini Serikali itapelekea fedha katika majimbo yao kwa ajili ya ujenzi wa vituo (stendi) vya mabasi vya wilaya.

“Waziri wa Mipango na Uwekezaji, nadhani hili nalo ni eneo mojawapo ofisi yako ilifanyie kazi kwa maana ya mipango nchi nzima. Wapi panahitaji stendi, wapi panahitaji soko kufanya hivyo uwekezaji wa hivi kila halmashauri kujua wapi panahitaji inakuwa rahisi fedha ikipatikana inaelekezwa nguvu huko,” amesema SpikaTulia.

Awali, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, aliwajibu wabunge hao akisema Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kujenga stendi hizo, huku akizitaka halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wake kisha serikali itamalizia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!