Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Tulia aingilia kati sakata wakuu wa shule waliosimamishwa kazi kisa Zuchu
Habari za Siasa

Spika Tulia aingilia kati sakata wakuu wa shule waliosimamishwa kazi kisa Zuchu

Zuchu
Spread the love

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ameagiza wakuu wa shule zilizoko wilayani Tunduma, Mkoa wa Songwe, waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kuwachezesha wanafunzi nyimbo iliyo kinyume na maadili, wapewe nafasi ya kusikilizwa na kama itabainika tukio hilo lilitokea wakati hawako shuleni, warudishwe kazini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Spika Tulia ametoa agizo hilo leo tarehe 6 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, akidai kuna taarifa zinazoonesha kwamba, wakuu hao wameadhibiwa bila kupewa haki ya kusikilizwa, lakini pia wakati tukio hilo linatokea walikuwa nje ya shule.

“Hatua za kinidhamu zina pande mbili, huyu kakosea ana haki ya kusikilizwa, aliyesimamishwa bila kusikilizwa utaratibu ukoje? Kama hakuwepo au alikuwepo tunaweza kuthibitisha tuseme sasa, lakini kama mamlaka ilitoa adhabu bila kujua na kama waliamua wakati hakuwepo shuleni na mamlaka ilichukua hatua bila kuwasikiliza warejeshwe kwenye nafasi zao,” amesema Spika Tulia

Akizungumzia agizo hilo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda, amesema walimu hao wanapaswa kukata rufaa ili tukio hilo liangaliwe upya.

“Hilo suala ni la kinidhamu, kama hawakuwepo wanapaswa kukata rufaa kwa mkurugenzi wa halmashauri. Kama mtu amechukuliwa hatua kinyume na utaratibu kama hakuhusika moja kwa moja anaruhusiwa kukata rufaa. Sisi tulitoa agizo kwa mkurugenzi achukue hatua,” amesema Prof. Mkenda.

Walimu hao walifukuzwa shule baada ya video kusambaa mitandaoni ikionesha wanafunzi wakicheza wimbo wa Honey, ulioimbwa na msanii Zuchu.

3 Comments

  • viongozi wa nchi hii wanakurupuka sana, nyinbo hazina maadili mazuri lakini zinachezwa kwenye media zetu, je tatizo ni la nan?? wanazipitisha hizo nyimbo kuchezwa kwenye media zetu au ni wanafunzi kucheza hiyo nyimbo

  • Mambo kama haya mnakuwa oyaoya sana kufuatilia ila mambo ya msingi mnajfanya mmefunga macho na masikio hebu acheni hizo tabia tufanye mambo ya msingi kwa ajili ya kujenga nchi sio kufuatiliana habari za nyimbo ety

  • Kisa walimu mbona hao waliochota ma tririoni ya fedha za Watanzania hawatajwi na kuchukuliwa hatua? Kwa nini waalimu wakati hata wao hawana maadili na uchungu kwa mali za umma? Wa.imu warejeshwe kazini hawana cha kujibu kwani matatizo yote huanzia kwao kwa kuruhusu mmomonyoko wa maadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!