Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai: Muulizeni Tundu Lissu swali hili  
Habari za SiasaTangulizi

Spika Ndugai: Muulizeni Tundu Lissu swali hili  

Job Ndugai
Spread the love

HATUA ya Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) kuandika taarifa ya kusitishiwa mshahara na stahiki zingine na Ofisi ya Bunge, imemsukuma Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri kuibuka na swali moja. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).  

“Naomba mumuulize Lissu swali hili, kama mwajiri hajakupa mshahara unaodai je, unakimbilia kwenye mitandao ya kijamii au utazungumza na mwajiri wako kwa taratibu zilizowekwa?” amehoji Spika Ndugai.

Spika Ndugai ametoa jibu hilo baada ya waandishi kadhaa kumpigia na kutaka kupata ufafanuzi wa madai ya Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge.

Ameongeza kuwa, Lissu aulizwe ni lini alikaa ama kupata muda wa kujadiliana na mwajiri wake kuhusu kusitishiwa mshahara na posho zake?

Pamoja na kutokuwa tayari kutoa maelezo mengi Spika Ndugai hajathibitisha moja kwa moja kama taasisi hiyo (Bunge) imesitisha mshahara na stahiki za Lissu ama la ambapo ameahidi kutoa ufafanuzi hapo baadaye.

Akizungumza na redio moja hapa nchini Spika Ndugai amesema, “wabunge ni kama waajiriwa wengine tu. Sio watu tofauti” na kwamba, wanapaswa kufuata utaratibu wa maeneo yao ya kazi.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa juu wa Bunge amesema kuwa, malalamiko ya Lissu hajayasikia wala kuyaona popote na kwamba, amekuwa akipigiwa simu kuulizwa jambo hilo.

Kauli ya Spika Ndugai kutopata malalamiko ya Lissu inaendana na ile iliyopolewa jana tarehe 14 Machi 2019 na Steven Kagaigai, Katibu wa Bunge wakati alipohojiwa na MwanaHALISI ONLINE.

Kagaigai alisema “malalamiko hayo sijayapata. Hata alipoulizwa kama ni kweli bunge limesitisha kutoa mshahara na posho za Lissu tangu Januari? Alijibu “malalamiko hayo hayajanifikia, mimi sijapata malalamiko hayo.”

“Leo napenda kuthibitisha kwamba uamuzi wa bunge kunifutia mshahara na posho zangu ulifanyika kabla hata ya Spika Ndugai kuombwa na kutoa mwongozo huo.

“Ndiyo kusema kwamba bunge la Spika, Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai limezuia mshahara na posho za bunge tangu mwezi Januari mwaka huu,” ilieleza sehemu ya taarifa ya Lissu aliyoisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Malalamiko ya Lissu kukata mshahara na stahiki zake zote za kibunge yametanguliwa na hoja iliyotolewa na Joseph Musukuma, Mbunge wa Geita Vijijini (CCM) katika Mkutano wa Bunge uliopita.

Musukuma aliomba mwongozo wa kiti cha Spika baada ya kupewa nafasi hiyo, alipakihoji kuwa ni lini Bunge litasitisha mshahara wa Lissu?

Kwenye maelezo yake Msukuma aliliambia Bunge kuwa, Lissu amepona na anazurura nje ya nchi na kutukana viongozi wa nchi, huku Bunge likiendelea kumlipa mshahara na posho.

Baada ya swali hilo, Spika Ndugai alisema “ni kweli, jambo hili la ndugu yetu, rafiki yetu, mbunge mwenzetu Tundu Antipas Lissu linahitaji kuangaliwa kipekee kwa maana ya kwamba mbunge hayupo jimboni kwake, hayupo hapa bungeni tunapofanyia kazi, hayupo hospitalini, hayupo Tanzania na taarifa zake Spika hana kabisa.

“Kwa maneno ya Mheshimiwa Musukuma, (Lissu) anazurura, kwa hiyo nikuhakikishie Mheshimiwa Musukuma, yale yaliyo ndani ya uwezo wangu nitayafanya. Asante kwa ushauri.”

Lissu yuko nje ya nchi tangu mwezi Septemba mwaka 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma.

Miongoni mwa sababu anazotoa Lissu kuhusu kutorejea kwake nchini hadi sasa ni matibabu. Baada ya kukumbwa na tukio hilo, Lissu alitibiwa katika hospitali zilizoko nchini Kenya na Ubelgiji.

Hata hivyo, amefanya ziara kadhaa huko ughaibuni ambapo tarehe tayari 19 Januari 2019 alihojiwa na Dira ya Dunia-Idhaa ya Kiswahili ya BBC.

Tarehe 21 Januari 2019 alihojiwa katika kipindi cha HardTalk (BBC) na mtangazaji maarufu Stephen Sackur ambapo tarehe 9 Februari 2019 kwa ajili ya mahojiano kuhusu demokrasia nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!