Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Spika Dk. Tulia awataka majaji wanawake kutenda haki
HabariHabari Mchanganyiko

Spika Dk. Tulia awataka majaji wanawake kutenda haki

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amewataka Majaji wa Mahakama nchini kuzingatia weledi, kufuata misingi ya kisheria na kutenda haki katika kazi zao.

Dk. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 16 Januari, 2023 wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) uliofanyika Mkoani Tanga kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa ni muhimu kuelewa kuwa siku zote mafanikio yao yasipimwe kwenye hukumu na maamuzi mangapi yaliyoandikwa na kutolewa tu, idadi ya vikao vya kesi walivyohudhuria au idadi ya mizozo iliyomalizika bali ni kwa jinsi gani nafasi zao katika Mahakama na maamuzi yametoa tafsiri katika kuiwezesha jamii kuondokana na ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake.

“Ni wakati wa kusimama imara kuweza kutimiza majukumu yenu hata pale kwenye vikwazo na changamoto za kijamii, kiimani na kitamaduni.

“Tukifanya hivyo, bila shaka tutakuwa sehemu ya kumwaga tone la maji litakalosambaa na kuwa dimbwi baadaye mto, ziwa na kuenea katika bahari kubwa ya jamii, na hivyo kufanya mwanamke kutoonekana Mhanga bali kuonekana Shupavu, Mpambanaji na Kiongozi,” amesisitiza Dk. Tulia

Sambamba na hayo, Spika amesema kuwa Bunge lake lipo tayari kupokea maoni ya mabadiliko ya sheria zilizopitwa na wakati ili kuzifanyia maboresho kwa lengo la kuhakikisha haki za makundi mbalimbali katika jamii zinalindwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!