WATU karibu 60,000 wamefariki dunia nchini China kwa Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), kati ya tarehe 8 Desemba 2022 hadi tarehe 12 Januari mwaka huu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Januari 2023 na Mkuu wa Tume ya Kitaifa ya Afya China (NHC), Jiao Yahui, watu 5,503 walifariki dunia kwa kushindwa kupumua, huku 54,435 walipoteza maisha kutokana na kuwa na magonjwa mengine tofauti na UVIKO-19.
Mitandao ya kimataifa imeripoti kuwa, vifo hivyo vimeongezeka baada ya China kusitisha utekelezaji wa sera yake ya kutokomeza ugonjwa huo ulioibuka 2019.
Akitoa taarifa hiyo, Yahui amesema asilimia 90.1 ya watu waliopoteza maisha walikuwa na umri wa miaka 65.
Leave a comment