Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika afafanua uamuzi wake kutowafukuza Mdee, wenzake bungeni
Habari za Siasa

Spika afafanua uamuzi wake kutowafukuza Mdee, wenzake bungeni

Spread the love

 

Spika wa Bunge la Tanzania Dk.Tulia Akson, ametoa ufafanuzi zaidi kuhusu uamuzi wake wa kutowafukuza bungeni wabunge 19 wa Chadema baada ya kupokea barua kutoka kwa chama hicho kumjulisha kuwa wabunge hao si wanachama wa chama hicho. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Tulia amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya mjadala mkali kuibuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uamuzi wake huo alioutoa asubuhi.

Baaadhi ya watu walihoji kwanini Spika ajizuie kufanya maamuzi kabla hata ya zuio la Mahakama kutolewa juu ya maombi ya wabunge 19.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu tarehe 16 Mei, 2022, Dk. Tulia amesema amechukua uamuzi huo mara tuu baada ya kujulishwa kuhusu uwepo wa kesi na yeye mwenyewe kujiridhisha.

Amefafanua zaidi kuwa Katiba inaeleza kuwa Mahakama ndiyo chombo cha mwisho cha uamuzi ikiwa mbunge ni halali au la.

Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson

Amesema kwa kutambua hivyo mara baada ya kufahamu kuwa kuna kesi juu ya uhalali wa wabunge hao hawezi kuwafukuza hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi wa kesi hiyo.

“Kwa mbunge ambaye amefuata taratibu zote za kuapishwa na akawa mbunge bila kujali ni wajimbo au Viti Maalumu anapokuwa amefukuzwa ubunge na kwenda kufungua kesi mahakamani anaendelea kuwa na sifa hadi hapo mahakama itakapokuwa imetoa amri.

“Mimi kazi yangu ni kutangaza na mahakama itakapotamka kuwa hawana sifa ya kuwa wabunge, mimi nitatangaza n ahata wasingeenda mahakamani kupinga ningetangaza kwamba nafasi zipo wazi,” amesema.

Alipoulizwa juu ya wabunge wa CUF ambao walifukuzwa ubunge huku kesi ikiendelea hadi leo amesema kuwa “naomba tujielekeze kwa yaliyotukia sasa kwasababu muda ni mchache.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!