October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mazungumzo yaanza kuwaondoa wanajeshi waliojeruhiwa Mariupol

Spread the love

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema kuwa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanawaondosha wanajeshi wao, waliojeruhiwa katika jimbo la Mariupol. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa mitandao … (endelea).

Ikumbukwe kwamba Urusi inataka kuchukua udhibiti wa mji wa Mariupol ambao wamekuwa wakiupigania kwa makombora kwa miezi kadhaa sasa.

Zelensky ametoa kauli hiyo, katika matangazo ya kila wiki ambayo amekuwa akiyatoa tangu kkuanza kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi yake.

Wakati huohuo, vikosi vya Ukraine vilivyopo karibu na Mariupol vilijificha katika kiwanda cha chuma wakati vikosi vya Urusi vilipowashambulia.

Hata hivyo, jeshi limetoa wito wa msaada baada ya wanajeshi wengi kujeruhiwa,’’ hapakuwa nan jia ambayo wangeweza kuitumia ili kutoroka katika eneo hilo, kwasababu jeshi la Urusi lilikuwa limezingira eneo hilo.’’

Katika hotuba ya Rais Zelensky, amesema kuwa wameanza mazungumzo ya kuangalia iwapo kama vikosi vya Urusi vitaruhusu kuwaondoa majeruhi.

Lakini Zelensky ameongeza kuwa mazungumzo hayo nimagumu sana.

Aidha hakuwataja wawakilishi wa Ukraine katika mazungumzo hayo, lakini amesema ni wao waliotaka yaanzishwe.

error: Content is protected !!