Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa
BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the love

Kiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza nepi kwa ajili ya watoto wachanga nchini humo na badala yake kitaangazia soko la watu wazima. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Oji Holdings ndiyo kampuni ya hivi punde imefanya mabadiliko kama hayo katika nchi ya Japan yenye idadi kubwa ya wazee, ambapo viwango vya kuzaliana viko chini sana.

Mauzo ya nepi za watu wazima yalizidi yale ya watoto wachanga nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Idadi ya watoto waliozaliwa nchini Japan mwaka 2023 – 758,631 – ilipungua kwa 5.1% kutoka mwaka uliopita.

Pia ilikuwa idadi ndogo zaidi ya watoto waliozaliwa katika rekodi nchini Japan tangu karne ya 19. Katika miaka ya 1970, idadi hiyo ilikuwa zaidi ya milioni mbili.

Katika taarifa, Oji Holdings ilisema kampuni yake tanzu, Oji Nepia, kwa sasa inatengeneza nepi milioni 400 za watoto wachanga kila mwaka.

Uzalishaji umekuwa ukishuka tangu 2001, wakati kampuni ilipofikia kilele chake cha nepi milioni 700.

Huko nyuma mwaka wa 2011, mtengenezaji mkuu wa nepi nchini Japan, Unicharm, alisema mauzo yake ya nepi za watu wazima yamepita yale ya watoto wachanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

error: Content is protected !!