Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini
Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the love

WANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara, wako mbioni kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama, baada ya mradi wa usambazaji huduma hiyo kutoka Ziwa Victoria unaogharimu Sh. 4.42 bilioni, kuanza kutekelezwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Mkataba wa utekelezaji mradi huo kati ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na mkandarasi Kampuni ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, kusainiwa tarehe 20 Machi 2024.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo (CCM), ameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wake, ambapo hadi sasa kiasi cha Sh. 1.44 bilioni, kwa ajili ya matumizi ya kazi za awali.

“Mradi huu utakapojengwa watakaoanza kusambaziwa itakuwa ni nyie na baada ya nyie wanaenda kule Kiriba katika vijiji vitatu. Nichukue nafasi hii kumshukuru Rais Samia kwa kutenga fedha hizi lakini pia nitoe wito kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili ukamalike kwa wakati,” alisema Prof. Muhongo.

Mwakilishi wa mkandarasi, Pius Amos, alisema kampuni yake itahakikisha ujenzi wa mradi unakamilika kwa wakati ili maji yaanze kusambazwa kwa ajili ya kuwafikia wananchi.

“Tumeshakabidhiwa mradi wa maji ambao tunaenda kuanza utekelezaji ndani ya wiki moja inayokuja. Tutaanza kuleta mitambi na vifaa vya ujenzi na tunategemea tutakamilisha ujenzi wake ndani ya muda uliopangwa au chini yake sababu tuna uzoefu katika suala hilo,” alisema Amos.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!