May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simulizi watano familia iliyouawa kikatili inasikitisha, RC, RPC wacharuka

Wilaya ya Bahi

Spread the love

 

WATU watano katika kijiji cha Zanka Wilayani Bahi mkoani Dodoma wameuawa katika nyumba waliokuwa wakiishi kijiji hapo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Waliouawa walitajwa kuwa ni Hosea Kapande (mume), Paulina (mke) pamoja na watoto wawili ambao wanafunzi Isaka (kidato cha kwanza) Agnes (darasa la tatu Agnes) na Helton (darasa la nne) ambaye ni mjukuu wa Hosea.

Taarifa za mauaji hao zinadaiwa kugunduliwa na watoto wadogo waliotumwa kwenda kufungua ndama jirani na nyumba hiyo juzi saa 10.00 jioni baada ya kusikia harufu ikitokea nyumba waliokuwa wakiishi marehemu hao.

Akizungumza juzi usiku, Mwenyekiti wa Kijiji cha Zanka Yohana Japhet alisema alipata taarifa hizo baada ya kupigia simu na wadogo za marehemu ambapo aliwapigia simu polisi na kisha kwenda eneo la tukio.

Naye Mdogo wa marehemu Hosea, Noah Kapande alisema saa 10.00 jioni juzi akiwa katika duka lake miili hiyo ndipo alisogea mahali zilipokuwa zikisikika na kuelezwa kuwa kaka na familia yake wamekutwa wamefariki wote.

Alisema baada ya hapo waliwapigia simu viongozi wa kijiji na watu wengine ndio wakaanza kukusanyika kwenye nyumba hiyo iliyopo kijijini hapo.

Mdogo wake Jackson Kapande alisema akiwa anakunywa soda dukani, alipata ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kutoka kwa mwanaye ukimtaka kumpigia simu.

“Nilivyopiga nikakutana na sauti makelele, nikamuuliza kuna nini mwanangu uko wapi akaniijbu niko huku kwa baba mkubwa njoo haraka,” alisema.

Alisema alikimbia alipofika akawauliza watu waliokuwa wamekusanyika kulikuwa na nini ndipo alipojibiwa kuwa kuna watu wameuawa huku na harufu zilikuwa zikisikika.

Alisema walipofungua ndani ya nyumba hiyo walikutana na maasi hayo yaliyopoteza familia nzima iliyokuwa ikiishi kwenye nyumba hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka aliwataka wakazi wa kijiji hicho pamoja na ndugu kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili waliofanya kitendo hicho wajulikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Hili jambo litakuwa limefanywa kwa ushirikiano na watu wa hapa, hawezi kuja mtu kutoka huko akaja kwenye nyumba ya mtu akauwa watu watano asiwe na mwenyeji hapa,” alisema.

Aliagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama na uchunguzi vyote mkoa kuhamia katika kijiji hicho kufanya uchunguzi wa tukio hilo na waone namna ya kushirikiana na wenzao kama italazimika kufanya hivyo.

“Ni lazima hawa watu wapatikane ni lazima. Labda wananzaka muwe wanafiki naomba wananchi wako watoe ushirikiano…Hii ni damu ya watu watajisema tu,”amesema.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga alisema madaktari wanafanyaia uchunguzi miili hiyo na hivyo baada ya uchunguzi huo watakuwa na nafasi ya kusema kuwa watu hao waliuawa katika hali gani.

“Mauaji yametokea na ni ya kikatili sana, sisi kama polisi tunaendelea kufanya uchunguzi tunatarajia tutawapata waliohusika na hili tukio lakini kwa sasa ni haraka mno kusema nani kahusika moja kwa moja na mauaji hayo,” alisema.

error: Content is protected !!