Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makinda awaangukia viongozi wa dini kuhamasisha sensa
Habari za Siasa

Makinda awaangukia viongozi wa dini kuhamasisha sensa

Kamishna wa Sensa na Makazi ya Watu Tanzania, Anna Makinda
Spread the love

 

KAMISHNA wa Tume ya Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda amewaomba viongozi wa dini kupitia Jumuiya ya Maridhiano kuwahamasisha Watanzania kushiriki kikamilifu zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Makinda ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Januari, 2022 wakati akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano jijini Dodoma.

Amesema anaamini viongozi wa Jumuiya hiyo wataisaidia serikali katika kuwahamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uandikishaji wa sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini mwaka huu.

Amesema viongozi hao wana nafasi kubwa ya kushawishi na kuwahamasisha watu kujitokeza kwa wingi ili kushirikia zoezi hilo muhimu ambalo kwa ajili ya maendeleo ya watanzania kiuchumi.

Aidha, amewataka watanzania pia kutoa ushirikiano katika utoaji wa majibu sahihi kwa watumishi watakaowaandikisha huko majumbani na maeneo mengineyo ili kupata idadi kamili ya watu na makazi yao.

Waziri Mlkuu Mstaafu, Mizengo Pinda

Naye, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha pia na viongozi wa ngazi mbalimbali ya serikali, amezitaka familia ambazo zina watoto wenye ulemavu kutowaficha pindi zoezi la uandikishaji wa sensa ya watu na makazi utakapofanyika mwaka huu.

Amesema tabia ya kuwaficha watu hao wenye ulemavu itaisababishia serikali kutowatambua watu wake.

“Itashindwa kufikia malengo yake ya bajeti itakayopangwa kwa ajili ya maendeleo ya watanzania na pia inawanyima haki yao ya kimsingi ya kuhesabiwa kama ilivyo kwa watu wengine.

“Itasikitisha kama kutatokea familia zenye watu ambao wanaoishi na walemavu wakawaficha na kusababisha wasihesabiwe, jamani hao nao ni watu kama sisi tulio wazima hivyo nitoe rai, kwa familia hizo ziwe tayari kutoa idadi kamili ya watu wanaoishi nao,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, Alhaji Sheikh Mussa Salumu amesema lengo kuu la jumuiya ni kuhakikisha amani ya Tanzania inadumishwa na kulindwa kwa gharama yoyote.

Amesema kwa kushirikiana na serikali, Jumuiya hiyo itahakikisha amani inadumishwa kwa dini zote ili watanzania waweze kufikia malengo yao kiuchumi na maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!