Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Wataalam 422 wapigwa msasa anwani za makazi
Michezo

Wataalam 422 wapigwa msasa anwani za makazi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Jim Yonazi akizungumza kwa njia ya mtandao (video conference) na wataalam kutoka Halmashauri mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar wakati akifunga mafunzo hayo katika ofisi za TTCL, jijini Dodoma.
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Jim Yonazi amefunga mafunzo ya utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi kwa njia ya mkutano mtandao kwa wataalam wa Tanzania Bara na Zanzibar yaliyofanyika kwenye vituo vinne vya mkoa wa Mwanza, Mbeya, Tanga na Zanzibar. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Yonazi amewataka wataalam hao 422 waliopatiwa mafunzo hayo ambapo wataalam 389 wametoka Tanzania Bara na 33 wametoka Zanzibar kwenda kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo kwa kuweka namba za nyumba, majina ya mitaa na barabara kwenye halmashauri wanazotoka ili kuhakikisha kuwa anwani za makazi zinatekelezwa nchi nzima na kukamilika ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Ameongeza utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi utasaidia kufungua kasi ya uchumi, utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi na kuifungua Tanzania kidijitali.

“Mwananchi yeyote atatambulika duniani na anaweza kufikiwa na mteja kwa ajili ya kuuza bidhaa au huduma, hivyo kila mwananchi awiwe kuwa na namba ya nyumba, jina la barabara au mtaa anapoishi,” amesema Dk. Yonazi

Pia, ametoa wito kwa kampuni, wadau mbali mbali na familia kuchangia utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi.

Amesema kila mmoja awe balozi wa anwani za makazi na wataalam watoe taarifa kwa viongozi wao na wizara hiyo iko tayari kuendelea kushirikiana kutekeleza mpango huo.

Naye Mratibu wa Kitaifa wa Anwani za Makazi na Postikodi wa Wizara hiyo, Mhandisi Jampyion Mbugi amesema wataalaam waliopatiwa mafunzo hayo ni wataalam wawili kutoka kwenye kila halmashauri nchi nzima.

Amesema mafunzo hayo ya wiki moja yamehusisha wataalam wa TEHAMA, Ardhi, Mipango Miji na Ramani.

Amesema kuanzia tarehe 17 Januari mwaka huu, utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi umeanza ikiwemo kuweka namba za nyumba, jina la mtaa au barabara na kuweka taarifa za maeneo hayo kwenye mfumo wa kielektroniki wa NAPA.

Amesema anwani zitawasaidia wananchi kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta bila changamoo yeyote.

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya wataalam wengine waliopatiwa mafunzo hayo, Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Kilindi –Tanga, Anastius Manumbu amesema kwa kupitia mafunzo hayo kwa vitendo na wataenda kuwafundisha wataalam wengine ili kuhakikisha kuwa anwani za makazi zinakamilika kwa wakati kuendana na malengo ya Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!