May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba wazindua jezi zao mpya

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imetangaza kuwa leo tarehe 3 Septemba 2021 jezi zake zitakazotumika katika msimu ujao wa mwaka 2021/2022 zitaanza kuuzwa rasmi. Anaripoti Damas Ndelema na Wiston Josia, TUDARCo … (endelea)

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Ofisa habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga amesema jezi hizo zitaanza kupatikana katika maduka yote ya Vunja bei nchi nzima.

Amesema Simba imefikia hatua hiyo baada ya kuwepo kwa maombi mengi ya jezi kutoka kwa mashabiki wa timu.

“Hivyo, uongozi umeona kuwasikiliza mashabiki na wapenzi wa timu ni jambo jema na jezi hizi zitauzwa kuanzia Sh. 25000 hadi Sh. 35000,” amesema.

Aidha, akizugumzia kuhusu kuvuja kwa jezi hizo, Kamwaga alisema “suala la jezi kuvuja ni la kawaida hata timu kubwa za barani Ulaya jezi zao huvuja hivyo huu ulikua ni mpango wetu wa kuzindua jezi na kuvuja kwa jezi sio kitu kwani kama jezi ni nzuri lazima watu watanunua na kuvaa jezi za timu yao.”

Kamwaga amesema kelekea Simba Day, kauli mbiu au Slogan itakayotumika ni “one team one dream. Tukimalizia na asubuhi tu twendeni wenye nchi.”

Amesema katika wiki ya Simba itakayoanza tarehe 13 hadi 19 Septemba, 2021 kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazowawezesha mashabiki wa Simba kunapata burudani.

Pamoja na mambo mengine Kamwaga litangaza viingilio katika kilele cha siku hiyo ya Simba.

“Zamani kulikua na utaratibu wa kutangaza vingilio siku chache kabla ya tukio jambo lililopelekea baadhi ya mashabiki kukosa tiketi, hivyo mwaka huu tumeona tutoe taarifa mapema kwa kutaja bei ya viingilio ili kuepusha usumbufu kwa mashabiki wetu.

Ezekiel Kamwaga, Kaimu Afisa Habari wa Simba

“Viingilio vitakua kama ifuatavyo; mzunguko Sh. 5,000, VIP A Sh. 20,000, VIP B Sh. 30,000, PLATNUM Sh 200,000 na tiketi zitaanza kuuzwa leo hii,” amesema.

Kamwaga aliongeza kuwa baada ya kumaliza kutangaza na kuuza tiketi p[amoja na jezi, jambop litakalofuata ni kuwajulisha mashabiki wa timu hiyo kuwa ni sehemu gani itaweka kambi.

“Kuhusu timu ya kucheza nayo siku ya Simba day, napenda kuwajulisha kuwa ni timu  kubwa Afrika ambayo ilishabeba Ubigwa wa Afrika  zaidi ya mara tatu… hivyo itakua mechi itakuwa sio ya kitoto  ili kumfanya kocha aone sehemu zenye changamoto na kuzipatia majibu,” amesema.

error: Content is protected !!