September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nape: Serikali itoe mikopo kwa wanafunzi kidato cha tano, sita

Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya Maposeni, Ruvuma, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mtihani

Spread the love

 

MBUNGE wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameitaka Serikali kutoa mikopo kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita kama ilivyo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo … (endelea).

Akiuliza swali la nyongeza kwenye swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Chumbuni, Ussi Salum Pondeza (CCM) kwamba Serikali haioni kuwa umefika wakati wa wanafunzi wote kunufaika kwa asilimia 100 bila kujali shule alizosoma.

Akijibu swali hilo la Nape leo tarehe 3 Septemba jijini Dodoma, Naibu Waziri wa elimu, Omary Kipanga alisema ni kweli vijana wa kidato cha tano na sita wanalipa ada ambapo kwa wanafunzi wa kutwa wanalipa Sh 35,000 wakati bweni wanalipa Sh 70,000, hivyo serikali inaona ni ni gharama nafuu.

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM)

“Watanzania wengi wanaweza kuimudu kuilipa lakini kama wizara pamoja na serikali tutaishughulikia kwa kina ili kipindi kijacho tutoe elimu bure pia hadi kwa ngazi ya kidato cha tano na cha sita kama ilivyo sasa kwa kidato cha kwanza hadi cha nne,” alisema.

Aidha, akijibu swali la Pondela, Kipanga alisema mikopo inayotolewa na serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inaongozwa na sheria ya bodi hiyo sura 178  mbayo inaelekeza kuwa walengwa wa mikopo hiyo ni wahitaji.

“Kwa sasa, uhitaji wa wanafunzi hupimwa kwa kuchambua taarifa zilizowasilishwa wakati wa maombi ya mkopo, ikiwemo gharama za masomo ya sekondari au stashahada,” alisema.

error: Content is protected !!