May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wafanyakazi 7,000 GGML waipaisha Geita 

Spread the love

ZAIDI ya wafanyakazi 7,000 walioajiriwa kwenye kampuni ya uchimbaji wa madini Geita (GGML) wameupaisha mkoa wa Geita baada ya michango yao katika michahara kusaidia ujenzi wa madarasa, shule na zahanati. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Pia Kampuni hiyo ambayo inatajwa kama mlipa kodi mkubwa na mwajiri bora hapa nchini, kila mwaka inaajiri vibarua 700 kutoka katika mitaa mbalimbali ya mji wa Geita.

Akifafanua kuhusu mchango wa kampuni hiyo katika kipindi cha miaka 21 iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Richard Jordinson amesema pia zaidi ya wakandarasi 3000 wamefaidika na uwepo wa kampuni hiyo.

“Mwaka huu tunaadhimisha miaka 21 ya GGML tangu ilipoanza kufanya kazi hapa Geita. Tunajivunia kusema kwamba mnamo 2020, asilimia 86 ya manunuzi yetu yote yalifanywa nchini Tanzania. Tumetoa ajira za moja kwa moja 5,067, pamoja na ajira za kudumu 1,842 na wafanyakazi 177 wa mikataba ya muda.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson

 “Kwa kuongezea, tunafanya kazi na wakandarasi 3,330 ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wetu wa kitaifa kupitia ushuru kwa njia ya mishahara, michango ya hifadhi ya jamii na uwekezaji mwingine,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema wafanyakazi – 700 wa kawaida (vibarua) wanaajiriwa kila mwaka na GGML chini ya mpango maalum unaoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na serikali za mitaa.

Alisema wafanyakazi hao wamechangia sana katika ujenzi wa miradi muhimu katika maeneo yao.

“GGML inaajiri vibarua zaidi ya 700 kila mwaka ambao huajiriwa kutoka mitaa mbalimbali inayoizunguka kampuni yetu. Wafanyakazi hawa wanalipwa kila mwezi na wanachangia sehemu ya mshahara wao kwa shughuli za maendeleo katika mitaa yao, ambayo hutumiwa kwa ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa, zahanati na shule, ” alisema.

Aidha, Mwenyekiti wa Mtaa wa Manga katika Halmashauri ya Mji wa Geita, Elias Lukanya, alishukuru GGML kwa msaada wao kwa jamii wenyeji kwani wafanyakazi hao wamefanya kazi nzuri katika maeneo yao.

“Vibarua hao wametuwezesha kujenga ofisi ya kisasa, zahanati, vyumba vya madarasa na nyumba ya mwalimu wetu. Serikali pia inatuunga mkono katika kukamilisha miradi hii,” alisema na kuongeza kuwa

“Ninatoa wito kwa uongozi wa halmashauri yetu kuujumuisha Mtaa wa Manga katika bajeti ya shilingi bilioni 9.2 zinazotumiwa kila mwaka na GGML kupitia mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii.

error: Content is protected !!