June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sheikh Farid: Nilitishwa

Shekhe Farid Had

Spread the love

 

SHEIKH Farid Had, mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam visiwani Zanzibar (JUMIK) alipokuwa gerezani Zanzibar, ameeleza alitolewa kauli za vitisho. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, kabla ya kuhamishiwa Tanzania Bara, ofisa mmoja wa polisi alimfuata na kumwabia “mara hii tumekukoseni, lakini mkitoka nje, tutamalizana.”

Akizungumza katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam leo tarehe 25 Juni 2021, baada ya Swala ya Ijumaa, Sheikh Farid alisema, vitisho hivyo alivipata mwaka 2017 visiwani humo. Hata hivyo, hakutaja jina la ofisa huyo.

“Hatujui lakini Mungu atatusaidia, tunaomba mtuombee dua, tuzidishe dua, hivi nina safari ya kwenda Tanga. Tuombeeni du asana,” amesema.

Ameeleza, walipokuwa gerezani walikutana na mambo mengi, lakini hakuwa tayari kueleza mambo hayo na kutoa ahadi kuzungumza na waumini hao wakati mwingine atapopata nafasi.

Kiongozi huyo aliyekamatwa mwaka 2012 kwa tuhuma za ugaidi visiwani Zanzibar na baadaye kuhamishiwa Bara, akiwa na wenzake, alifutiwa mashitaka na Mkuregenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu tarehe 16 Juni 2021.

Akizungumza na waumini walioswali kwenye msikiti huo, Sheikh Farid amesema, Watanzania bila kujali dini zao walioesha mapenzi makubwa ya kutaka haki itendeke, kwamba kwa hilo wanawashkuru sana.

“Nimekuja kutoashukrani zangu kwenu, Hivyo mmetunusurunkwa kadri mlivyo weza. Sio nyinyi tu, hata wasio Waislaam wamestaajabisha kwa kuona dhulma ile haikubaliki.

“Mmetunusuru kwa kadri mlivyoweza. Sio nyinyi tu hata waio wauslaam kuwastaajbusa hata wasio Waislam kuona dhulma ile haikubaliki,” amesema.

Ameeleza, katika nchi yoyote uadilifu unapotamalaki, hutia baraka na kinyume chake nchi huingia kwenye giza na kwamba, kwa namna mwanadamu alivyoumbwa, hujua dhuluma na haki hata kama hajafundishwa.

Wafuasi kundi la Uamsho

“Uadilifu unatia baraka katika nchi lakini dhulma ikitanda katika nchi, inatia giza. Tunashuhudia mambo yakiendelea, yanasawazishwa mambo mengi sana yaliyopita. Tuwaombee dua wanaofanya haya.

“Usishangae kumkuta Muislam, Mkristo ama mla unga anasema wanawaonea Waislam, fikra ya mwanadamu inajua hili ni ovu,” amesema.

Alimeeza waumini hao kwamba, kulikuwa na michango mbalimbali na wengine kwenda kuwajulia hali gerezani, hivyo hawana cha kuwalipa na watalipwa na Mungu.

Kwa sauti ya chini Sheikh Farid amesema, baadhi ya Watoto wa wao walichukuliwa na majirani na kulelewa kama Watoto wao wa kuwazaa, na kwamba jambo hilo limewatia furaka mioyoni.

“Kilichojia hapa ni kuwashukuru Waislam, hatuna cha kuwalipa. Mmechangia misaada, ndugu zetu wamekuja kututembelea na dua nyingi walituombea, kuna wazee hawajapata hata kutuona lakini walikuwa wakituomba dua.

“Kuna watu waliwachukua watoto wet una kuwatunza kama Watoto wa kuwatoa kwenye matumbo yao, wamealea kwa miaka yote tulioyokuwa gerezani. Hakika hatuna cha kuwalipa,” amesema.

error: Content is protected !!