Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi wa Jamhuri: Nyaraka hizi alisaini Zitto
Habari za Siasa

Shahidi wa Jamhuri: Nyaraka hizi alisaini Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo (mwenye kanzu) akiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeendelea kusikiliza kesi Na. 237/2018 ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

 Leo tarehe 17 Mei, 2019, shahidi wa nne upande wa Jamhari ameelezwa kuwa ni Inspekta Salum Seif Masoud, mpelelezi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kinondoni.

Kwenye kesi hiyo, upande wa serikali umewakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga,Wakili wa Serikali Wankyo Simon na Janneth Magoho. Upande wa Utetezi umeongozwa na Wakili Peter Kibatala, Dickson Matata na Steven Mwakibolwa.

Wakili Katuga amemuongoza shahidi kutoa ushahidi wake mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kama ifuatavyo:-

Wakili Katuga: Shahidi ieleza mahakama unafanya kazi wapi?

Shahidi: Ofisi ya Mkuu wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni.

Wakili Katuga:Upo hapo kama nani?

Shahidi: Kama msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni na majukumu yangu ni kusimamia askari wa chini yangu pia nashughulika na makosa ya jinani na makosa ya mtandaoni.

Wakili Katuga: Upo hapo kwa muda?

Shahidi: Tangu mwezi Julai mwaka 2018.

Wakili Katuga: Hiyo ofisi ipo wapi?

Shahidi: Ipo kwenye Kituo cha Polisi Osterbay.

Wakili Katuga: Tarehe 31 mwezi Oktoba, 2018 mchana unakumbuka ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa eneo langu la kazi  Kituo cha Polisi Osterbay, nikiwa hapo nilikuwa kwenye shughuli zangu za kiupelelezi alikuja Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi akiwa na Mbunge Mheshimiwa Zitto Kabwe, kwasababu Ofisi ya Msaidizi ipo karibu na Mkuu wa Upelelezi, nilimuona aliingia naye ofisini kwake  kwa mahojiano.

Wakili Katuga:Wewe ulijua kwanini Zitto Kabwe yupo hapo  na kwa ajili ya nini?

Shahidi: Alikuja kwa ajili ya tuhuma anazokabiliwa nazo za kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya serikali, maneno ambayo aliyatoa tarehe 28/10/2018.

Wakili Katuga: Nini kimeendelea?

Shahidi: Nikiwa kama mpelelezi hilo jambo nilikuwa nalifahamu na alikiri kweli kuwa, huo mkutano aliufanya basi mimi nikamuomba (Press-Release) ya huo mkutano wake aliofanya na waandishi wa habari.

Hakimu Shahidi: Hapo wakati unamuuliza baada ya mahojiano na  RCO au uliingilia kati?

Shahidi: Baada ya kumalizana na RCO nikaomba (Press-Release).

Wakili Katuga: Mheshimiwa Zitto Kabwe yupo hapa mahakamani?

Shahidi: Yupo.

Wakili Katuga: Ni yupi?

Shahidi: Ni yule pale aliyekaa kizimbani.

Wakili Katuga: kwa ridhaa yako mheshimwa hakimu tunamuomba shahidi akumuoneshe Zitto.

Shahidi alikwenda kumshika bega zitto aliyesimama baada ya kuona shahidi anakwenda upande wake na mahojiano yakaendelea.

Wakili Katuga: Ni mahojiano ya aina gani yalifanyika kati huyu msaidizi wa RCO na Zitto?

Shahidi: Kuhusu mkutano wake na waandishi wa habari.

Wakili Katuga: Ulikuwa unasikiliza hayo mahojiano?

Shahidi: Nilikuwa nasikiliza.

Wakili Katuga: Na ulimuomba (Press-Release) baada ya Zitto kufanya kitu gani?

Shahidi: Baada ya kukiri kuwa alifanya mkutano.

Wakili Katuga: Baada ya kumuomba hiyo (Press-Release) alijibu nini?

Shahidi: Alijibu haina shida kwa kuwa pale hakuwa nayo alimuagiza kijana wake aje nayo.

Wakili Katuga: Iambie mahakama kama ilitokea ikapatika?

Shahidi: Baada ya muda kidogo, huyo kijana alikuja na hiyo Statement na kumkabidhi Mheshimiwa Zitto.

Wakili Katuga:Wewe kama wewe uliweza kujua hiyo nyaraka imefuatwa wapi?

Shahidi: Hapana, sikuweza kujua ila Mheshimiwa Zitto baada ya kuipitia alisema ndio yenyewe.

Wakili Katuga: Iambie mahakama ilichukua muda gani?

Shahidi: Nilipomuomba haikuchukua muda sana.

Wakili Katuga: Unaweza kukumbuka?

Shahidi: Siwezi kukumbuka.

Wakili Katuga: Ulikabidhiwa lini?

Shahidi: Siku hiyo hiyo tarehe 31 baada ya hapo nilimwambia aisaini.

Wakili Katuga: Ilikiwa wapi?

Shahidi: Kituoni Osterbay.

Wakili Katuga: Baada ya hapo?

Shahidi: Mimi baada ya kuipitia nikaipitia nikamuomba asini kuwa amenikabidhi hiyo na mimi nikasaini kwa kuwa, tulikuwa askari wengi nikamuomna mmoja aje awe shahidi.

Wakili Katuga:Unaweza kumkumbuka huyu mwenzako?

Shahidi: Ndio, Gabriel Katengu baada ya hapo nikamkabidhi incharge wa upelelezi Albart.

Wakili Katuga: Hiyo unayoita hiyo hati ya makabidhiano ya hiyo Press –release?

Shahidi: Ndio, kuna saini yangu na saini zitto Kabwe.

Wakili Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama angalia hiyo nyaraka.

Wakili Katuga: iangalie na iambie mahakama kuwa hiyo ndio hati ya makabidhiano uliyoitaja?

Shahidi: Ndio kuna saini yangu kuna saini ya Zitto.

Wakili Katuga: Iambie mahakama hiyo nyaraka unataka waifanye nini?

Shahidi: Waipokee kama kielelezo.

Wakili Katuga: Hiyo Press-Release utaikumbuka?

Shahidi: Ndio.

Wakili Katuga: Utaikumbuje?

Shahidi: Inakurasa sita ina nembo ya chama cha ACT- na mwishoni kuna siani ya Mheshimiwa Zitto Kabwe ilikuwa Headline ‘Serikali imevuruga zao la Korosho, imeshindwa kulinda ustawi na usalama wa raia’.

Wakili Katuga: Iambie mahakama hizo page (kurasa) zilikuwa za namna gani?

Shahidi: Ilikuwa ina kurasa nyeupe na maandishi meusi.

Wakili Katuga: Kwa ridhaa ya mahakama angalia nyaraka hii?

Shahidi: Anaangalia (Press-Release).

Wakili Katuga: Hiyo ni nini shahidi?

Shahidi: Hiyo ndio nyaraka aliyonikabidhi Zitto.

Wakili Katuga: Unataka mahakama iifanye nini?

Shahidi: Iiridhie na iichukue kama kielelezo.

Wakili Katuga: Shaidi isome hiyo nyaraka.

Katka kesi hiyo Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kutenda tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Chama cha ACT wazalendo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 18 na 19 mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!