April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Membe, Musiba kukutana Julai 2

Spread the love

MAKAHAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imepanga tarehe 2 Julai 2019 kutoa uamuzi wa madai ya fidia ya Sh. 10 bilioni, ya kesi iliyofunguliwa na Bernard Membe, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje dhidi ya Cyprian Musiba. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).  

Mahakama hiyo mbele ya Jaji Jocqwine Demela leo tarehe 17 Mei 2019, imepanga tarehe hiyo baada ya mawakili wa pande zote mbili,  Wakili Majura Magafu anamtetea Musiba na Wakili Johnathan Mndeme anayemwakilisha Membe, kusikilizwa hoja zao.

Upande wa walalamikiwa uliwasilisha maombi namna 119/2019 ya kuomba kuongezewa muda wa kuwasilisha majibu yake nje ya muda.

Katika kesi hiyo Musiba, anayejitambulisha kama mwanaharakati na mtetezi wa Serikali na Rais John Magufuli, anatuhumiwa na Membe kwamba, anamhujumu Rais Magufuli, ikiwa ni pamoja na kufanya kampeni za kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

error: Content is protected !!