Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi nilipigwa jiwe na wafuasi wa Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi nilipigwa jiwe na wafuasi wa Chadema

Spread the love
  1. MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea kusikiliza ushahidi kwenye kesi ya Uchochezi nambari 112 ya mwaka 2018,  inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema), ambapo mahakama hiyo imesikiliza shahidi wa nne. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 31 Mei 2019, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba upande wa Serikali uliongozwa na wakili Faraja Nchimbi, Paul Kadushi, Wankyo Simon na Jackline Wantori  ulimuongoza shahidi wao aliyejitambulisha kuwa ni askari polisi H7856 PC Fikiiri Mgeta mwenye miaka 28.

Katika kesi hiyo upande wa utetezi umewakilishwa na Wakili Pater Kibatala, Jeremiah Mtobesya, John Mallya, Dickson Matata na Hekima Mwasipu.

Mtuhumiwa namba moja kwenye kesi hiyo ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama hicho, Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Z’bar.

Wengine ni Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Vijijini, Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na John Heche, Mbunge wa Tarime vijijini.

Wakili Jackline alimuungoza shahidi kutoa ushahidi wake mahakamani hapo na kueleza majukumu yake, PC Fikiri aliieleza mahakama kuwa kazi yake ni kulinda raia na mali zao akitekeleza majukumu yake katika kituo cha Polisi cha Osterbay kilichopo wilayani Kinondoni.

PC Fikiri ameieleza mahakama kuwa  aliajiriwa na jeshi la Polisi mwaka 2015, elimu yake ni muhitimu wa kidato cha nne na alijiunga na chuo cha mafunzo ya polisi Moshi.

Alipoulizwa anakumbuka nini siku ya terehe 16 Februari, 2018 alijibu kuwa, alikuwa kwenye majukumu na alipangiwa doria eneo la Mwananyamala kwa Kopa na ilipofika majira ya saa 11 kuelekea saa 12 walipewa taarifa na kiongozi wao wa doria, Sajenti Hamadi aliyepata taarifa kupita radio-call ya polisi  iliyowataka waelekee Mkwajuni ambapo kulikuwa na kusanyiko.

Anadaiwa kuwa walikwenda  eneo la tukio kwa kupita njia za vichochoro hadi kufika kwenye eneo la tukio na kuona mkusanyiko wa watu waliokuwa kwenye barabara ambapo anakadiria kufikia hadi watu 500 au 600 na barabara zilifungwa na watu hao.

Anadai kuwa kusanyiko hilo lilikuwa linaviashiria vya uvunjifu wa amani na kwamba watu hao walifunga barabara bila utaratibu pia walikuwa wameshika mikononi  mawe, fimbo, chupa walizojaza mchanga, chupa za maji lakini pia kulikuwa na uhamasishaji uliokuwa ukiashiria uvunjiafu wa amani.

“Nyimbo walizokuwa wakiimba pale ni kwamba hatupoi hatuogopi hatuogopi bunduki mtatuua na nyimbo nyingine wakiwa na hali ya jazba,” anadai kuwa wao walipofika pale walisikia Ilani ya Polisi ikitamkwa wakiwa kwenye gari aina Toyota Land Cruiser.

Ameileza mahakama kuwa ilani ilitamkwa “Kwa jina la Rais wa Muungano wa Tanzania ili lile kusanyiko litawanyike kwa amani,” ambapo anasema kuwa watu wale aliwaona kuwa ni wafuasi wa Chadema na viongozi wao aliowaona wakiwa mbele wakihamasisha kusonga mbele huku wakikaidi Ilani hiyo.

Anadai kuwa aliwatambua kuwa hao ni viongozi wa Chadema kwa kuwa kashawahi kuwaona kwenye shughuli za kisiasa na kwenye kampeni na bungeni.

Ameeleza kuwa wafuasi wa Chadema aliwatambua kwa sababu walivaa sare za chama hicho na wakati huo kulikuwa na mwanga wa kutosha kuweza kuona kinachoendelea na kwa makadirio ya umbali aliokuwa yeye na waandamanji ni kama mita 20.

Anadaiwa kuwa kwenye maandamano hayo alimtambua Mbowe, Mdee, Msigwa na Mwalimu.

Ameleeza kuwa wafuasi wa Chadema wakihamasishwa na viongozi wao walisonga mbele huku wakikaidi ilani ya Polisi na hatimaye wakaanza kurusha chupa mawe na miti hapo ndio afande Ngichi Mkuu wa Operesheni aliamuru kutumiwa kwa mabomu ya machozi lakini askari mmoja alipigwa jiwe la shingo na kudondoka chini wakati  wanamsaidi naye alipigwa jiwe na mkono.

“Nilivaa saa mkono wa kulia sikujua saa yangu imeenda wapi ghafla nikapigwa jiwe na kichwa nikapata maumivu makali,” ameelesa PC Fikiri.

Ameeleza kuwa yeye na mwenzake aliyemtaja kuwa ni PC Rahimu walikimbizwa katika Hospitali ya Polisi ya Kilwa Road na walitibiwa hapo kwa siku tatu

Alilazwa kuanzia siku ya tarehe 16 hadi 18 Daktari alimpa ruhusa na kupewa mapumziko ya wiki mbili. Baada ya hapo aliionesha mahakama fomu ya matibabu ya PF3 na kitambua na kuiomba mahakama iipokee ili iwe kama kielelezo mahakamani

Hakimu Simba aliipokea fomu hiyo.

Itaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!