November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shahidi apiga ‘yowe’ baada ya kubanwa na Wakili

Spread the love

MASHAKA Juma, shahidi wa pili kwenye kesi inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameieleza mahakama kuwa, wakili anambana kwenye maswali. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Mashaka wakati akitoa ushahidi wake awali alieleza kwamba, alikuwa ameguswa na maneno ya Zitto na hata kulichukia Jeshi la Polisi kutoka na ukatili waliotendewa wananchi kwa mujibu wa kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi,  shahidi huyo aliulizwa maswali na upande wa utetezi juu ya ushahidi alioutoa.

Yafuatayo ni mahojiana ya shahidi huyo na wakili wa utetezi, Peter Kibatala:-

Wakili Kibatala: Unasema weweni msanii wa filamu, msingi wa fani yako ni kuigiza?

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba, wakati wa kazi yako inabidi kuna mazingira unatakiwa uigize umefiwa, unalia kabisa kiasi ambacho anayeona ajue umefiwa kweli?

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Bila shaka wakati mwengine unaigiza umekasirika sana?

Shahidi: Haina shida ndio kazi yangu

Wakili Kibatala: Na unasemea kuwa, unipenda hiyo kazi na sasa unayo kwa miaka 10?

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Kazi zako ulizoigiza kama nilikusikia vizuri ni Utata na Wazee wa Pamba, uligiza uhusika mbalimbali?

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Nikisema wewe ni mzoefu wa sana, maigizo nitakuwa sawa?

Shahidi: Hujaharibu

Wakili Kibatala: Wakati unatoa ushahidi ulisema wewe ni mkazi wa Kimara Korogwe, sahihi?

Shahidi: Sahihi

Wakili Kibatala: Unakumbuka kusema chochote kuhusu hii Kimara Korogwe ipo wapi?

Shahidi: Ipo Korogwe

Wakili Kibatala: Aha sawa ipo Korogwe?

Shahidi: Ipo Dar es Salaam

Wakili Kibatala: Wakati unatoa ushahidi wako ulikumbuka kusema ulikuwa wapi?

Shahidi: Najibu nilichoulizwa

Wakili Kibatala: Ukimuacha huyu Frank Zonga, hawa wengine uliwataja majina?

Shahidi: Sijawataja

Wakili Kibatala: Ulisema sehemu gani unacheza drafiti, ni bar, nyumbani kwako au barabari?

Shahidi: Sijasema sehemu gani

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba, hiyo Youtube na hiyo simu ni ya Frank Zongo?

Shahidi: Eee! ndio mmliki wa hiyo simu?

Wakili Kibatala: Shahidi wewe unamiliki Smart phone humiliki?

Shahidi: Namiliki

Wakili Kibatala: Ina YouTube haina YouTube?

Shahidi: Hapana Sijadownload

Wakili Kibatala: Ni shahihi Youtube ni Applicationi unayoweza ku-download kupita Play-store?

Shahidi: Sina utaalamu huo

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba, hiyo Youtube ilikuwa ni Frank Zongo ?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili Kibatala: Ulisema kuhusu mahali anapoishi Frank Zongo?

Shahidi: Sijasema

Wakili Kibatala: Ni sahihi kuwa, hujawahi kuingia kwenye simu yako kuthibitisha yale uliyoyaona kwa Frank Zongo?

Shahidi: Nithibitishe nini sasa, nilichokiona ndicho nilichokiamini

Wakili Kibatala: Ni sahihi pia kuwa shahidi huyu mtu ambaye hujamtaja majina yake alichukua simu ya Frank Zongo?

Shahidi: Rudia

Wakili Kibatala: Ulisema chochote kuhusu huyu mtu nayeye aliona kile ulichokuonesha  Frank Zongo?

Shahidi: Tulikuwa wote

Wakili Kibatala: Ulisema chochote kuhusu huyu mtu kuchukua simu ya Frank Zongo kwenda nayo Polisi Osterbay?

Shahidi: Sikusema

Wakili Kibatala: Ulisema chochote huyu mtu kuhusu kuchuku namba ya Frank Zongo?

Shahadi: Hajachukua namba

Wakili Kibatala: Ulisema chochote kuhusu huyu mtu kuongea na lile kundi la watu pale?

Shahidi: Aliongea na mimi kama mimi, hajachukua.

Wakili Kibatala: Hukusema chochote kuhusu huyu mtu uliyekuwa unaongea naye pembeni kama alirudi kuongea au lile kundi lenu?

Shahidi: Mimi nilikuwa naongea kama mimi

Wakili Kibatala: Ulisema chochote kuhusu unaishi mtaa gani na mjumbe wako ni nani?

Shahidi: Sijaulizwa

Wakili Kibatala: Ulisema unaka wapi?

Shahidi: Kimara Korogwe, Kirungule

Wakili Kibatala: Ulisema?

Shahidi: Sijasema

Wakili Kibatala: Ulisema kuhusu mwenyekiti wako wa mtaa?

Shahidi: Sijasema

Wakili Kibatala: Ulisema chochote kuhusu jerani yako mpangaji wako au baba mwenye nyumba wako?

Shahidi: Hilo sikusema

Wakili Kibatala: Unafahamu unatoa ushahidi kwenye kesi ya Jinai?

Shahidi: Nafahamu

Wakili Kibatala: Uliongozwa kusema chochote kuhusu kutoa kitambulisho chochote ili na mimi niamini kuwa naongea na Mashaka?

Shahidi: Nilikuwa na kitambulisho cha mpiga kura kimepota

Wakili Kibatala: Umetoa au hujatoa?

Shahidi: Sijatoa

Wakili Kibatala: Kitambulisho chako ni cha mpiga kura lesseni au?

Shahidi: Cha mpiga kura

Wakili Kibatala: Ulikipataa lini?

Shahidi: Sikumbuki mwaka gani ila nilikipata

Wakili Kibatala: Ushawahi kusikia kuhusu lost- report?

Shahidi: Kiswahili chake

Wakili Kibatala: Waraka wapolisi kupotea kwa kitambulisho au chochote

Shahidi: Nilipewa

Wakili Kibatala: Ulipewa kituo gani na lini?

Shahidi: Magomeni

Wakili Kibatala: Lini?

Shahidi: Sikumbuki nakumbuka nilipoteza hiko na kamera

Wakili Kibatala: Uliutoa huo waraka (Lost-report) mahakamani?

Shahidi: Sikuitoa

Wakili Kibatala: Shahidi wewe huko Zitto alipofanya mkutano na waandishi ulikuwepo?

Shahidi: Sikuwepo, niliona kwenye youtube

Wakili Kibatala: Hii Lost-report uliipata kabla au baada ya hii tukio

Shahidi: Kabla

Wakili Kibatala: Wakati unakuja hapa ulisindikizwa na polisi

Shahidi: Sahihi

Wakili Kibatala: Ulisindikizwa na polisi wenye sare  na asiyekuwa na sare?

Shahidi: Mimi nilipofika hapa unanielewa ee

Wakili Kibatala: Nakuelewa

Shahidi: Nilifika mapokezi

Wakili Kweka (Wakili wa Jamhuri)Mawakili tusitake majibu tunayotaka sisi, tunamuomaa msomi mwenzangu ampe shahidi nafasi.

Wakili Kibatala: Eehe ulipofika mapokezi?

Shahidi: Nilipokelewa nikaambiwa subiri kuitwa

Wakili Kibatala: Uliwaona polisi wenye sare?

Shahidi: Sikuwaona

Wakili Kibatala: Na wale waiokuwa na sare?

Shahidi: Siwezi kujua, mimi nitajuaje kama huyu polisi au huyu sio polisi?

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba, ulipoenda Osterbay kutoa maelezo ulishaona hili tukio?

Shahidi: Sasa utatoleaje maelezo kitu ambacho hujakiona?

Wakili Kibatala: Pale Osterbay Ulikwenda na nani? labda mzazi au Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa?

Shahidi: Mimi mwanaume najiamini

Wakili Kibatala: Ulipokwenda kutoa ushahidi, ulikuwa na amani na ukatoa ushahidi kwa roho safi?

Shahidi: Naomba wakili asinipe sana kibano, nitakosa kutoa vitu Mheshimiwa Hakimu?

Hakimu: Shahidi wewe mjibu

Wakili Kibatala: Nakuuliza tena ulipokwenda polisi Osterbay ulikuwa na amani?

Shahidi: Kama nilivyokueleza kuwa, nilikwenda nikiwa nawachukia polisi

Wakili Kibatala: Ulipokwenda, ulikwenda huku unajua ulikuwa unawasiwasi labda uliwasiliana na jamaa yoyote kuwa nipo polisi lakini sina amani?

Shahidi: Huwa mimi ni mwanaume ninayejiamini

Kweka Wakili (Wakili wa Jamhuri): Maswali ya wakili ndio yanayomfanya shahidi kupaniki

Wakili Kibatala: Wakati unaongozwa na wakili, shahidi hebu tueleze alikuuliza swali lolote kuhusu wewe kuthibitisha hizi taarifa za hawa watu kuua?

Shahidi: Hapa hajaniuliza

Wakili Kibatala: Alikuuliza chochote kuhusiana na watu kutekwa?

Shahidi: Hajaniuliza

Wakili Kibatala: Labda na wewe ulipata muda wa kudhithibisha hizi taarifa?

Shahidi: Nilithibitisha nilipohojiwa

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba, hadi unafika hapa hujathibitisha kuwa haya matukio ya mauaji ya kweli?

Shahidi: Mimi sio mthibitishaji maana matukio yametokea Kigoma mimi sio polisi

Wakili Kibatala: Ni sahihi ulitaja tukio la kutekwa kwa Mo?

Shahidi:Tafadhali usiniingize kwenye matatizo (kwa sauti ya juu).

Wakili Kibatala: Ulimtaja ‘Mo’ tukio la kutekwa kwa Mo Dewji?

Shahidi: Ndo nilimtaka Mo si ndiye huyu kila mtu unamjua

Wakili Kibatala: Ulipata nafasi ya kuongea na Zitto?

Shahidi: Nitamuona wapi? nilimuona kwenye video.

Wakili Kibatala: Ulishawahi kuongea na Waziri wa Mambo ya Ndani kuhusiana na video hiyo.

Shahidi: Nitampata wapi?

Wakili Kibatala: Ulipata nafasi ya kuongea na Rais ndiye bosi wa Waziri na Mkuu wa Jeshi la Polisi?

Shahidi: Mheshimiwa sijapata nafasi ya kuongea Rais, kama Mheshimawa wakili atanipa njia nitafika nitashuku lakini ni ngumu kweli Mheshimiwa.

Wakili Kibatala: Ulipata nafasi ya kwenda kuuliza kwa msajili kuwa huyu ni Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo?

Shahidi: Nafikiri hata yeye hawezi kujitangaza kuwa ni kiongozi kama hajafuata taratibu.

Wakili Kibatala: Shahidi ulienda au hujaenda?

Shahidi: Kufuata nini?

Wakili Kibatala: Ulifanya zoezi la kumshika bega kwa kumtambua kuwa huyu ndio Zitto Kabwe?

Shahidi: Sijaruhusiwa mahakama ikiniruhusu nitaenda

Wakili Kibatala: Sahihi kuwa ni yule pale

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Ni sahihi ulisema yule pale amekaa hujasema amekaa kizimbani?

Shahidi: Sijasema lakini nimesema amekaa

Wakili Kibatala: Ukipata dharura ya kipolisi utaenda polisi na utaomba msaada wa polisi?

Shahidi: Ushasema dharura ya kipolisi, nitaenda polisi

Wakili Kibatala: Hapa nimeshika hati ya mashtaka, kuna shtaka la kwanza hapa nitalisoma ‘Watu waliokuwa majeruhi katika tukio la mapambano kati ya raia na polisi walikwenda kutibiwa kwenye Kituo cha Afya cha Nguruka, polisi waliwafuata na kuwauwa’ uliongozwa kuyasema kama nilivyoyasoma hapa?

Shahidi: Sijayasoma

Wakili Kibatala: Je haya maneno umeyasikia unakumbuka kuongozwa kuyarudia

Shahidi: Itakuwa ngumu

Hakimu Shahidi: Itakuaje ngumu?

Shahidi: Ametamka maneno ya kitaalamu kwanza mahakama itambue nina ubovu wa macho

Wakili Kibatala: Ni sahihi hata wewe mwenyewe hujaomba ruhusa haya maneno uyasome?

Shahidi: Mimi sina utaalamu sana wa kuyarejea kama ulivyo wewe mtaalamu wa mambo ya mahakama

Wakili Kibatala:…Tumekuwa tuliyafuatilia kwa kina taarifa za huko Uvinza… wengine wameuwawa kwenye purugushani na polisi’ iambie mahakama kwamba, maneno haya uliyasoma?

Shahidi: Sikuyasoma

Wakili Kibatala: Ni sahihi kwamba, sio wewe au mwendesha mashtaka aliyekumbuka kuyasoma maneno haya

Shahidi: Hata mahamakama inayajua

Wakili Kibatala: Unasema kuwa, mtu huyu alikuwa akicheza na nyie drafiti mara kwa mara?

Shahidi: Sahihi

Wakili Kibatala: Sio kwamba alikuwa akipita na gari yake alishuka alipowaona nyie

Shahidi: Hapana

Wakili Kibatala: Ni sahhi hujataka jina la huyo mtu

Shahidi: Sahihi

Wakili Kibatala: Namba zako za simu ulizitaja?

Shahidi: Nilizitaja

Wakili Kibatala: Ulitaja labda 07..?

Shahidi: Sijataja

Wakili Kibatala: Nilikusikia kwamba wewe ulimsifu Zitto kwa ujasiri?

Shahidi: Ndio

Wakili Kibatala: Umesema wewe unamshabikia Zitto Kabwe?

Shahidi: Sana

Wakili Kibatala: Umemfollow Facebook au Instagram

Shahidi: Sijamfollow lakini kuna aina nyingi ya urafiki unaweza usimfollow lakini ukawa unamkubali

Wakili Kibatala: Uliongozwa kutaja rangi ya kaunda suti uliyosema ameivaa aliyoivaa Zitto?

Shahidi: Sijasema.

Baada ya hapo Wakili Kweka alimsahisha shahidi kutokana na maswali aliyokuwa akiulizwa na upande wa utetezi.

Wakili Kweka: Wakati unaulizwa na wakili wa utetezi ulipomtaja ‘Mo’ ulimaanisha‘Mo’ gani?

Shahidi:Mohammedi Dewji, Mfadhili wa Simba.

Wakili Kweka: Wakili alikuuliza kuhusu video uliyoiona na simu iliyotumika ilikuwa simu gani?

Shahidi: Ilikuwa smartphone ni ngumu kusema namba ngapi?

Wakili Kweka: Ni ya nani?

Shahidi: Frank Zongo.

Wakili Kweka: Wakili alikuuliza kuhusu kitambulisha chako na jina lako unaiambia nini mahakama kuhusu jina?

Shahidi: Mimi ni mtanzania ndio maana nimekuja mahakamani.

Wakili Kweka: Kuhusu jina lakona mahakama utaithibitishia nini kuwa kweli hilo ni jina lako?

Shahidi: Hata ukienda Hospitali ya Ifakara utaliona Jina langu.

Wakili Kweka: Uliposema Zitto amekaa pale ulikuwa ukimaanisha nini?

Shahidi: Nilikuwa nikimaanisha yule aliyekaa pale na hata angekaa kwa ya watu ningehesabu watu ningekuambia yupo baada ya watu wangapi.

Wakili Kweka: Mahakamami umekuja kufanya nini?

Shahidi: Kueleza hisia zangu juu ya Jeshi la polisi.

Wakili Kweka: Nimemaliza

Hakimu Huruma: Kuna Jengine la kuniambia mimi?

Shahidi: Nalichulia sana Jeshi la Polisi, naomba mahamama yako initoe hofu juu ya Jeshi la Polisi.

Baada hapo upande wa Jamhuri umemleta wakili mwingine…

Itaendelea leo …

error: Content is protected !!