April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ang’oa wakurugenzi wawili wa Halmashauri

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe na Uyui mkoani Tabora. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, inaeleza kwamba Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Adelius Makwega na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Hadija Makuwani.

Taarifa ya Msigwa inaeleza kuwa, Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo tarehe 16 Mei 2019 katika kikao cha kazi, kati yake na Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu na Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Wakurugenzi wa Halmashauri hizo watateuliwa baadaye,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Msigwa.

error: Content is protected !!