July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Abass: Kutekwa watu hakujaanza sasa

Dk. Hassan Abbas, Katibu Mkuu wizara ya Habari

Spread the love

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abass amesema kuwa, matukio ya utekaji na kuotea kwa watu hayajaanza ndani ya Serikali ya Awamu ya Tano. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Na kwamba, matukio hayo yamekuwa yakitokea hata kabla ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kuingia madarakani.

Dk. Abass ametoa kauli hiyo leo tarehe 17 Mei 2019, wakati akihojiwa na Kituo cha Redio cha East Afrika.

Amesema, matukio ya kutekwa na watu kupotea yanatokea hata katika nchi zilizoendelea, na kwamba, miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa matukio hayo ni kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia.

“Katika nchi yoyote kadri mnavyoendelea, sayansi na teknolojia inaleta changamoto mpya. Suala la kupotea au kutekwa hizo ‘crime’ ambazo ukienda kwenye nchi zilizoendelea huwezi sema ni za kawaida lakini ni vitu mabavyo vinatokea,” amesema Dk. Abass.

Aidha, Dk. Abass amesema, matukio hayo yanaweza kusabishwa na uhusiano binafsi wa watu wanaokumbwa na matukio hayo.

“…Sababu mahusiano ya mtu na mtu wewe serikali yanakuhusu nini? mtu huko labda katapeli watu kafanyaje huwezi kujua, labda mwingine kazi yake inaweza ikasababisha changamoto akatengeneza maadui,” amesema Dk. Abass.

Hata hivyo, Dk. Abass amesema, serikali inaweka mifumo kuhakikisha raia wanakuwa salama, pia inaendelea kushughulikia matukio ya watu waliopotea kusikojulikana.

“Serikali inaweka mfumo kuhakikisha raia wanakuwa salama, lakini  kusema imeanza awamu ya tano watu kupotea si kweli. Nchi kubwa duniani watu wengi hupotea kwa sababu ni mahusiano.

Nchi zinavyoendelea wapora nao wanakuwepo, sisi kama nchi hiyo ni changamoto lazima tuifanyie kazi ili raia wawe salama na wananchi watoe ushirikiano,” amesema Dk. Abass.

error: Content is protected !!