November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatenga Mil 605 ukarabati Chuo Tango

Omary Kipanga, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania inaendelea na ukarabati wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, unaogharimu Sh. 605.2 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Omary Kipanga, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia leo tarehe 20 Aprili 2021, akijibu swali la Flatei Gregori Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini (CCM), bungeni jijini Dodoma.

Massay ameuliza, “serikali ina mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA katika Jimbo la Mbulu Vijijini ili vijana wapate ujuzi?”

Pipanga amesema, katika Wilaya ya Mbulu kuna Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Tango, ambacho pia kinatoa mafunzo ya ufundi stadi.

“Chuo hiki, kinaendelea na ukarabati na ujenzi wa miundombinu, utakaogharimu jumla ya Tsh.605 milioni ambao unatarajiwa kukamilika Juni, 2021.”

“Hivyo, katika kipindi hiki ambacho serikali inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani humo, nashauri wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini kuendelea kutumia vyuo vilivyopo nchini, ikiwa ni pamoja na Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi- Tango na Chuo cha VETA Manyara,” amesema.

Amesema, serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitenga jumla ya Tsh.48.6 bilioni kwa ajili ya kujenga vyuo 29 vya VETA, katika ngazi ya wilaya ambavyo kwa sasa vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

error: Content is protected !!