Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaja na mpango kufuga nyuki kisasa
Habari Mchanganyiko

Serikali yaja na mpango kufuga nyuki kisasa

Spread the love

Serikali inatarajia kuanzisha mpango wa ufugaji nyuki ujulikanao kama Manzuki ambapo nyuki watakuwa wanafugwa katika eneo maalum bila kuathiri uhifadhi. Anaripoti Urumasalu Kisung’uda, TUDARCo…(endelea).

Hayo yamesemwa jana tarehe 24 Agosti 2022 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela(wa nne kutoka kulia), Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini,Mhe. Doto Biteko (wa pili kutoka kulia) pamoja na viongozi wa Serikali na chama wakiwa katika mkutano na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kuhusu masuala ya uhifadhi na ufugaji nyuki.

Amefafanua kuwa kupitia mpango huo wananchi watafuga nyuki na kupata faida bila kuhama kuhama.

Kuhusu wananchi wanaofuga nyuki katika Hifadhi ya Kigosi, amesema kuwa Serikali imeruhusu wananchi kuendelea na shughuli za ufugaji nyuki wakati inatafuta eneo mbadala la kuwahamishia wafugaji hao.

“Tamko la Serikali ni kwamba shughuli za ufugaji nyuki zitaendelea hadi pale tutakapotoa mbadala wa wapi mpeleke mizinga yenu,” Masanja amesisitiza.

Aidha, amewataka wananchi kukitumia ipasavyo kiwanda cha kuchakata asali kilichopo katika eneo hilo ili waweze kuuza asali kwa faida.

Amewataka wananchi kutunza mazingira na kuacha kukata miti hovyo ili kuendelea kufaidika na mazao yatokanayo na nyuki.

Awali, Waziri wa Madini na Mbunge wa Bukombe Dk. Doto Biteko amesema, Rais Samia anataka kuona kero za wananchi wakiwemo wa Uyovu zinatatuliwa na ndiyo maana Naibu Waziri amefika, hivyo kuwasihi wananchi kuwa wahifadhi kwa kuilinda misitu ya Bukombe isiharibiwe.

Naibu Waziri huyo anaendelea na ziara yake katika Kanda ya Ziwa kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazoikabili Sekta ya Maliasili na Utalii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!