Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yagoma kufuta adhabu ya kifo
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yagoma kufuta adhabu ya kifo

Kitanzi cha kunyonga
Spread the love

PAMOJA na kilio cha muda mrefu kutoka kwa taasisi mbalimbali zinazotetea haki za binadamu cha kuitaka serikali kufuta adhabu ya kifo, bado adhabu hiyo itaendelea kutumika nchini kwa miongo mingine kadhaa. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).  

Hayo yamo kwenye taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), iliyowasilishwa jana Ijumaa, mjini Dodoma, mbele ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria.

Badala yake, serikali inaeleza katika taarifa yake kuwa imeimarisha upelelezi katika mashauri yanayohusina na mauaji.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyopewa jina la “utekelezaji wa mpango kazi wa kitaifa wa haki za binadamu (2013 -2017,” serikali imesema, kutofutwa kwa sheria hiyo, kumetokana na matakwa ya wananchi.

“Serikali ilikusanya maoni kuhusu haki ya kuishi kutoka kwa wananchi, ikiwamo uwezekano wa kufuta adhabu ya kifo. Wananchi waliowengi, wametaka adhabu hiyo iendelee kutumika,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo kwa Bunge.

Inasema, “wizara ya mambo ya ndani kwa kushirikiana na jeshi la magereza, inatekeleza jukumu la kuwarekebisha wafungwa walioko gerezani. Haya yanafanyika kupitia program mbalimbali, ikiwamo mafunzo darasani, michezo, ushauri nasaha na stadi za kazi.”

Aidha, taarifa inaeleza kuwa wizara inaendelea kusimamia mpango maalum wa kuwapo kwa adhabu mbadala badala ya kifungo gerezani na kwamba waziri wa katiba na sheria, kwa mamlaka aliyopewa ametoa msamaha kwa wafungwa 240 waliokuwa na matatizo ya akili.

Kuhusu mauaji ya vikongwe, ripoti inasema, serikali imefanikiwa kukomesha kwa kiasi kikubwa mauwaji ya wazee na watu wenye ualbino.

Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora, imetajwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano yam waka 1977 na imepewa mamlaka kwa sheria ya Bunge. Miongoni mwa kazi zake, ni usimamizi wa utawala bora na haki za binadamu.

Aidha, Tume imepewa mamlaka ya kuinua na kulinda haki za binadamu; kufanya uchunguzi juu ya kuwapo uvunjifu wa haki za binadamu, kutafiti, kuelimisha na imepewa mamlaka ya kumfungulia mtu, watu au idara yoyote ile, kesi mahakamani.

Kazi nyingine za Tume, ni kuomba fidia kwa ajili ya mwathirika wa uvunjaji wa haki za binadamu; na inaelekezwa kushirikiana na idara na vyombo vya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Madola na vyombo vingine vitakavyoanzishwa kwa makubaliano ya nchi mbili au zaidi.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, imepewa jukumu la kusaidia upatanishi na maridhiano baina ya pande mbili zilizoko katika mgogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!