Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump aitunishia misuli Iran, yajibu mapigo
Kimataifa

Trump aitunishia misuli Iran, yajibu mapigo

Donald Trump
Spread the love

BAADA ya Rais wa Marekani Donald Trump mwanzoni mwa mwezi Mei 2018, kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia na Iran wa mwaka 2015, ametangaza kuliwekea vikwazo vya kihistoria taifa hilo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Rais Trump jana tarehe 2 Novemba 2018 kupitia akaunti yake ya Twitter aliandika kwamba vikwazo vinakuja, huku taarifa ya Ikulu ya White House ikieleza kuwa, vikwazo hivyo pia vitalenga mataifa yanayoshirikiana na Irani katika masuala ya biashara.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya Ikulu ya White House, inaeleza kuwa vikwazo hivyo havitahusu mataifa nane ambayo haikutaja jina, yanayofanya biashara na Irani, hasa uingizaji wa mafuta kutoka katika nchi hiyo.

Vikwazo vipya na vya zamani vya Marekani dhidi Iran, vinatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumatatu ya Novemba 5 2018, ambapo vitaelekezwa katika sekta ya usafirishaji wa majini, taasisi za kifedha na biashara ya mafuta.

Katibu wa Hazina wa Marekani, Steven Mnuchin, aliongeza kuwa Iran itaondolewa na au kutengwa kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na mtandao wa malipo wa kimataifa wa Swifti kutoka mjini Brussels nchini Ubelgiji, kusitisha huduma kwa taasisi za kifedha kutoka Irani, kitendo kitakachoathiri mfumo wa kifedha wa kimataifa wa taifa hilo.

Kufuatia mzozo huo, Umoja wa Ulaya (E.U) umearifu kwamba utalinda mataifa yake yanayofanya biashara halali na Iran.

Katika taarifa yao ya pamoja, mkuu wa masuala ya kigeni wa E.U, Federica Mogherine na mawaziri wa masuala ya kigeni kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani na Ufaransa wamesema watalinda uchumi wa wa Ulaya hasa wa nchi zinazofanya biashara na Irani kwa mujibu wa sheria ya E.U na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 Iran yajibu mapigo kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje, Bahram Qasemi alinukuliwa na kituo cha luninga cha taifa hilo, akisema kuwa Iran ina ujuzi na uwezo wa kusimamia vyema masuala yake ya kiuchumi, na kwamba hakuna uwezekano wa Marekani kufanikisha matakwa yake ya kisiasa kupitia vikwazo hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!