Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Nondo aachiwa huru kesi ya kujiteka
Habari MchanganyikoTangulizi

Nondo aachiwa huru kesi ya kujiteka

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Iringa leo imemkuta Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Leo Novemba 5 mwaka 2018 Hakimu Liad Chamshama amemuachia huru Nondo baada ya upande wa Mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yake mahakamani hapo.

Nondo alishitakiwa kwa kesi ya msingi ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Ushahidi wa Jamhuri

Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi wake mahakamani hapo uliopelekea kumtia hatiani Nondo pamoja na ushahidi wa ofisa upelelezi wa makosa ya mitandao ambaye pia ni shahidi namba tano, koplo Abdulkadir ambaye alidai mahakamani hapo kuwa Nondo alikuwa akiwasiliana na Mange Kimambe Mtanzania anayeishia Marekani.

Koplo Abdukadir alidai kuwa alipokuwa akiifanyia uchunguzi simu ya Nondo alinasa mawasiliano yake na Mange Kimambe ya tarehe 25 Februari mwaka huu ambapo alieeleza“Ujumbe huo pia ulisema, amepata tetesi kuwa anatafutwa na watu wasiojulikana na kushauriwa asitembee peke yake kwa sababu ana hatihati ya kutekwa,” alidai koplo Abdulkadir.

Pia aliieleza mahakama hiyo kuwa Nondo alituma ujumbe saa 9:09 mchana siku ya tukio kwa kutumia simu ya mkononi kupitia mtandao wa Whatsap kwenda ka Paul Kisabo akiwa Ubungo uliosomeka “am at risk” .

Shahidi huyo alidai alikuta namba tatu za simu ambazo hazikupokewa katika simu ya Nondo ambazo zilipigwa kati ya saa nane mchana hadi 3:45 usiku.

Shahidi namba mbili koplo John alisema alimpokea mshtakiwa huyo katika Kituo cha Polisi Mafinga na kuandikisha maelezo yake.Koplo huyo alisema baada ya kuchukua maelezo hayo alibaini kuwa Nondo hakutekwa kama upelelezi wa koplo Abdulkadri ulivyobaini na hivyo waliamua kuripoti suala hilo katika uongozi wa juu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!