Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yabanwa mgawo wa umeme, yaomba uvumilivu hadi Feb. 16
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yabanwa mgawo wa umeme, yaomba uvumilivu hadi Feb. 16

Spread the love

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewaomba Watanzania waendelee kuvumilia makali ya mgawo umeme hadi tarehe 16 Februari mwaka huu ambapo majaribio ya uzalishaji wa umeme kutoka katika Bwawa la Mwalimu Nyerere yatakuwa yamnekamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema baada ya majaribio hayo, wanategemea  kuanza kupata megawati 215 za mwanzo hivyo umebaki muda mchache ukilinganisha na hali ilivyokuwa huko nyuma.

Abubakar Assenga

“Tuvumilie ili tuweze kukamilisha zoezi hili ili kupata umeme wa uhakika,”  amesema.

Kapinga ametoa kauli hiyo leo Alhamisi bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge waliolalamika mgawo wa umeme katika majimbo yao licha ya mvua kunyesha na kusababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani (Chadema) alihoji je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza changamoto ya kukatika kwa umeme Wilaya ya Nkasi.

Akijibu swali hilo Kapinga amesema wilaya ya Nkasi inapata umeme kupitia njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 66.

Amesema kwa kutambua changamoto ya kutokujitosheleza kwa umeme, Serikali imeshaanza mradi wa kupeleka umeme kutoka Gridi ya Taifa kwa Mkoa wa Rukwa ambapo mkoa utapata umeme kupitia utekelezaji wa Mradi wa TAZA ulioanza kutekelezwa Novemba, 2023 na unatarajiwa kukamilika Agosti, 2026.

Judith Kapinga

Hata hivyo, katika swali la nyongeza Khenani alihoji nini sababu nyingine ya umeme kukatikatika katika maeneo mbalimbali ya nchi licha ya serikali kudai changamoto ya kukatika kwa umeme inatokana na upungufu wa maji ambayo sasa maji ni mengi na mafuriko yametokea.

Naye Mbunge wa Mbagala, Abdallah Chaurembo (CCM) alihoji Serikali iweke wazi ni nini sababu za msingi za kukatika kwa umeme katika eneo hilo.

Pia Mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga (CCM) alidai licha ya eneo lake kuwa na migopi ya Kidatu na Kihansi ya kuzalisha umeme cha ajabu kuna tatizo la mgawo wa umeme.

Aidha, Mbunge wa viti maalumu CCM, Stella Fiyao naye alidai kila mara umeme unakatika Songwe licha ya kuwa mkoa jirani na nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika ambako biashara imepamba moto.

Akijibu maswali hayo, Kapinga alisema maeneo ya mabwawa ya kuzalisha umeme hayakupata mvua za el nino hapo awali,  ambapo kiwacho cha uzalishali kipungua kutoka Megawati 426 hadi 254 lakini sasa kwa mvua zinazoendelea uzalishaji umeongezeka hadi Megawati 400.

Aida Khenani

Amesema kiujumla kuna upungufu 144 lakini Serikali inaendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme nchini.

Kuhusu Mbagala naibu waziri huyo amesema kwa kuwa ni eneo linalokua kwa kasi wameagiza mashine ili kutanua kituo cha kupoza umeme pamoja na kuimarisha miundindombinu, vivyo hivyo kwa upande wa Kilombero amesema Serikali inatarajia kujenga kituo cha kupoza umeme.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

error: Content is protected !!