Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wanawake walalamikia ukubwa kondomu za kike, waomba zipunguzwe
AfyaTangulizi

Wanawake walalamikia ukubwa kondomu za kike, waomba zipunguzwe

Spread the love

Wataalamu wa afya wilayani Ileje mkoani Songwe wameagizwa kuanza kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu za kike ambazo zimelalamikiwa na  baadhi ya watumiaji wanawake wa kondomu hizo kuwa ni kubwa kuliko maumbile yao.

Pia wanawake hao wameiomba Serikali kupitia ofisi ya mganga mkuu wa halmashari ya wilaya hiyo, kupunguza ukubw wa kondomu hizo ili wazitumie kwa uhuru na kuisaidia jamii kukabiliana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwango Virusi Vya Ukimwi (VVU). Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Kondomu za kike

Agizo hilo limetolewa jana tarehe 31 Januari 2024 katika kikao cha baraza la madiwani la hlamshauri ya Ileje baada ya kuibuka kwa ajenda ya wanawake wilayani humo kuogopa kutumia kondomu hizo kutokana na ukubwa wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Ukimwi ambaye ni Diwani wa kata ya Itale, Fahari Mwampashi amesema hofu ya watumiaji wa kondomu hizo ni kwamba wanasema kubwa ikilinganishwa na maumbile yao.

Fahari amesema wanawake wengi wilayani huo wameomba zipunguzwe ukubwa.

“Wanawake wanaogopa kuvaa hizo kondomu za kike wakidai zitabakia ndani na kuhatarisha afya zao, huku wengine wakiomba wataalamu wa afya kupitia ofisi ya mganga mkuu kuwekeza nguvu ya utoaji elimu,” amesema Mwampashi.

Naye Diwani viti maalumu, Vema Rungwe amesema matumizi ya kondomu za kike, ukubwa wake na uvaaji ni changamoto hasa ikizingatiwa hakuna msukumo wa kuzitangaza kwa jamii ili kuleta uelewa badala yake hamasa kubwa imewekezwa kwa upande wa kondo za kiume pekee.

Madiwani na wataalam wa halmashauri ya Ileje wakiwa kwenye kikao cha baraza wakijadili mambo mbalimbali.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ubatizo Songa amesema ili kutekeleza mkakati wa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi, wataalamu wa afya wanatakiwa waendelee kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kondomu za kike na kiume ili jamii iwe na uelewa sahihi wa matumizi yake.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya Ileje, Joyce Ongati amekiri kuwepo kwa changamoto ya matumizi ya kondomu za kike kwa wanawake licha ya elimu kutolewa na kuahidi kuendelea kuongeza juhudi za elimu zaidi.

Mmoja wa mwananchi waliozungumza na MwanaHALISI Online,Mariamu Shimwela amesema awali waliletewa kondomu hizo lakini wanaogopa kuzitumia kwa hofu ya maumbile yao kuwa madogo walikilinganisha na ukubwa wa kondomu zilivyotengenezwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!