September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali ya Tanzania yamwita kumhoji Balozi wa Marekani

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania, imemwita Kaimu Balozi wa Marekani nchini humo, Dk. Imni Patterson ili kumhoji juu ya masuala mbalimbali ambayo ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho ikiwemo ugonjwa wa COVID-19. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 26 Mei 2020 na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Tanzania, Emmanuel Buhohela imesema, mazungumzo kati ya Balozi Imni na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Kanali Wilbert Ibuge yamefanyikia ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Buholela amesema, katika mazungumzo hayo, Kanali Ibuge ameonyesha masikitiko yake juu ya taarifa ambazo Marekani imekuwa ikizitoa kuhusu usafiri kwa raia wake.

Katika taarifa hiyo, inasema, Kanali Ibuge ametolea mfano wa taarifa zilizotolewa na Marekani katika mtandao wa Twitter tarehe 13 na 25 Mei, 2020 kwa raia wake ukielezea hali ya corona jijini Dar es Salaam si nzuri.

Kanali Ibuge amesema, taarifa hizo zinaelezea jinsi hospitali za jiji la Dar es Salaam vilivyosheheni wagonjwa wa corona ilihali si kweli jambo, jambo linaloweza kuleta taharuki kwa Watanzania na raia wengine wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali.

Katibu mkuu huyo, amemtaka Balozi Imni kutoa taarifa zilizothibitishwa kwani Tanzania haina kizuizi chochote kwa mabalozi wanaohitaji taarifa hizo.

Katika mazungumzo hayo, Kanali Ibunge ametumia fursa hiyo kumshukuru Balozi hiyo kwa ushirikiano anaoutoa na kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani.

error: Content is protected !!