October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dereva wa IT aliyewapa lifti watu wane, nusura auawe

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto

Spread the love

JESHI la Polisi jijini Dodoma limeeleza, kuwa dereva wa gari namba T.237 DSJ aina ya Subaru (IT), aliyewapa lifti watu wawili waliokuwa wakienda Kahama, wakiwa njiani walimgeuzia kibao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akizungumza na wahabari leo tarehe 26 Mei 2020, Gilles Muroto, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amesema, watu hao walimtolea silaha na kumtisha dereva huyo, walimkamata na kumfunga kamba na kisha walimtupa vichakani nao wakatokomea na gari hilo.

“Gari namba T.237 DSJ aina ya Subaru (IT), ilikuwa ikisafirishwa kwenda Uganda, dereva alipakia abiria wawili Misugusugu, Pwani ambao walikuwa wakienda Kahama, Shinyanga lakini matoke yake dereva alitishiwa silaha na kuporwa gari huku wakimwacha wamemfunga kamba na kutupwa porini eneo la Pandambili, Kongwa.

“Tulifanya ufuatiliaji kwa kushirikiana na wenzatu wa Pwani na kufanikiwa kulikamata likuwa huko Kiwanga Bagamoyo, Pwani. Lilikuwa na namba bandia, tumekamata watuhumiwa sita,” amesema bila kutaja jina.

Amesema, jijini humo walifanya msako wa siku nne mfululizo na kufanikiwa kukamata magari 17 yanayodaiwa kuibwa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Kamanda Muroto amesema, polisi walifanya msako ndani ya mkoa na mikoa mingine ya jirani, na kubaini magari hayo 17 kuwa na dosari na kudhaniwa yameibwa.

Amesema, magari hayo yamekutwa na kadi pia mafaili ya magari mengine. Pia yamekatwa ‘chesesi’ za kuungwa kwenye magari mengine huku mengine yakiwa na namba tofauti tofauti.

“Magari haya yana utata na kuna maswali mengi ya kujiuliza, kwanini gari ibandikwe chesesi isiyo yake? na kwanini magari yanabatizwa namba nyingine? Kwa hiyo ukifuatilia kwa undani, utagundua kuwa haya magari ni ya wizi.

“Tumeamua kufanya msako ili kukomesha kabisa tabia ya wizi isiendelee ndani ya mkoa wetu, na nashauri watu wafanye kazi hakuna njia ya mkato,” amesema.

Akitaja baadhi ya watuhumiwa na magari waliyokamata amesema, Helman Stephen alikamatwa akiwa na gari namba T.891 BXY, Toyota Premio na kuwa, gari hilo linatumia kadi na usajili wake.

“Mwami Monya (42), mfanyabiashara na mkazi wa Mpamaa,
Miyuji alikutwa akitumia gari namba T.680  BWU aina ya Toyota Prado, lenye Chassis Namba RZJI 200626277 na injini namba 3RZ3204070, lakini linatumia usajili wa kadi na jalada la gari lingine,”amesema.

Abdallah Mavumila, amekamatwa akiwa na gari T.866 DFT aina ya Alphad, gari hilo linatumia usajili wa kadi ya gari lingine ambazo siyo zake.

Kamanda Muroto amesema, gari namba T.926 Mitsubish Fuso lenye chesesi namba FH217C502904, amekutwa nalo Mwami Monya (42), mfanyabiashara na mkazi wa Mpamaa Miyuji Dodoma.

Mwami Mwaluganje (42), mkazi wa Miyuji Dodoma yeye amkutwa na gari namba T.450 AST Scania lenye chesesi namba Y5ZPE6X4Z01206603 ikisoma taarifa tofauti na kadi ya gari  hiyo.

Thomas Tesha, amekamatwa na gari T.992BAK aina ya Fuso, huku Bakari Omary akiwa na gari T.383 CXF na kwamba taarifa zake zinatofautian.

error: Content is protected !!