
SERIKALI ya Tanzania inatarajia kupokea ndege nyingine mpya toleo la Airbus A220-300 itakayotua nchini Jumapili Desemba 23, 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbas ameeleza hayo leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
“Ungana nasi kuipokea ndege ya kwanza kununuliwa na Serikali kwa toleo la Airbus A220-300. Ni Tanzania pekee.’Ngorongoro-Hapa kazi Tu’, itawasili nchini Jumapili hii na siku chache baadaye ndege nyingine kama hiyo itawasili Dodoma-Hapa Kazi Tu,” ameandika Dk Abbas.
Rasmi:Ungana nasi kuipokea ndege ya kwanza kununuliwa na Serikali ya Afrika kwa toleo la Airbus A220-300. Ni Tanzania pekee. Ngorongoro-Hapa Kazi Tu itawasili nchini Jumapili hii na siku chache baadaye ndege nyingine kama hiyo DODOMA-Hapa Kazi Tu itawasili.#TUNATEKELEZA2018 pic.twitter.com/lqHHUtJISI
— Msemaji Mkuu wa Serikali (@TZMsemajiMkuu) December 21, 2018
Tumeshakabidhiwa mali yetu, karibu nyumbani Twiga wa Ngorongoro, karibu nyumbani A220-300 Airbus.#TUNATEKELEZA2018 pic.twitter.com/2Q7ii9OqFB
— Msemaji Mkuu wa Serikali (@TZMsemajiMkuu) December 21, 2018
More Stories
Uchaguzi wa wanawake Chadema waingiliwa
Dk. Mwinyi amteua Dk. Mkuya, Nassor Mazrui
Waziri Majaliwa aitaka TPA kuongeza umakini