
Akram Aziz, akitoka mahakamani Kisutu
NDUGU wa mfanyabiashara mashuhuri nchini, Rostam Aziz, anayefahamika kwa jina la Akram Aziz, amefutiwa mashitaka na serikali. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Akram alifunguliwa mashitaka mahakamani tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Alituhumiwa kukutwa na nyara za serikali, ujangili, utakatishaji wa fedha, udangaanyifu na kujimilikisha silaha kinyume cha sheria.
Mbele ya Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, upande wa mashitaka uliwasisha hoja ya kumfutia mtuhumiwa huyo mashitaka yote yaliyokuwa yanamkabili.
Hata hivyo, alizuiwa kuondoka mahakamani hapo. Inadaiwa kuwa serikali imepanga kubadilisha hati yake ya mashitaka ili kuweza kumfungulia mashitaka mengine.
More Stories
Mapadri 25, Masista 60 waaga dunia Tanzania
TCRA yajitosa bei za vifurushi
Huawei yaunga mkono malengo endelevu UN