Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali kuiwezesha DMI vifaa vya kisasa na majengo
HabariHabari Mchanganyiko

Serikali kuiwezesha DMI vifaa vya kisasa na majengo

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa uchumi wa bluu unaoendelea jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Chuo cha Bahari (DMI).
Spread the love

 

SERIKALI imeahidi kukiwezesha Chuo cha Bahari (DMI), cha jijini Dar es Salaam kwa miundombinu bora na vifaa vya kisasa vya kufundishia ili kiweze kuwa na viwango vya kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ahadi hiyo ilitolewa leo Jumanne jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, wakati akifungua kongamano la kwanza la uchumi wa bluu.

Kongamano hilo lililoandaliwa na DMI ni la kwanza kufanyika nchini kuhusu uchumi wa bluu na maudhui yake ni ‘Kuibua fursa zitokanazo na bahari kwa maendeleo ya taifa’.

Alisema eneo kilipo chuo hicho Posta Dar es Salaam ni dogo sana hivyo serikali inaangalia uwezekano wa kutenga eneo kubwa kwenye Mkoa wa Pwani kwaajili ya kupanua shughuli za chuo hicho.

Washiriki wa mkutano wa uchumi wa bluu wakiteta jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaoendelea jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Chuo cha Bahari (DMI).

Alisema kwa kuanza serikali imeshatenga Sh bilioni moja kwaajili ya ununuzi wa mfumo wa kufundishia ma nahodha wa meli inayofahamika kama Stimulators.

“Niliwahi kutembelea hiki chuo hivi karibuni na kwa kweli nilijionea mwenyewe miundombinu ilivyo chakavu lakini mkakati uliopo ni kukiwezesha kuwa cha kisasa na kitakuwa na majengo yenye viwango na kwa kuwa wana maeneo makubwa Mkoa wa Pwani itakuwa kazi rahisi kwetu ,” alisema Mwakibete

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya DMI, Ernest Bupamba, aliiomba serikali iiangalie DMI kwa jicho la huruma ikizingatiwa kuwa ndicho chuo pekee kinachotoa mafunzo  ya bahari hapa nchini.

Alisema chuo hicho ndicho pekee kinazalisha rasilimali watu inayohitajika kwenye uendeshaji wa uchumi wa bluu hivyo iwapo kitawezeshwa kwa vifaa na majengo kitatoa mchango mkubwa kwenye kufikia malengo yaliyowekwa kwenye uchumi huo.

Washiriki wa mkutano wa uchumi wa bluu wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa uchumi wa bluu ulioandaliwa na Chuo cha Biashara DMI

Aliishukuru serikali ya visiwa vya Shelisheli kwa namna ambavyo imeisaidia Tanzania katika kupambana na vitendo vya uvuvi haramu kwenye bahari yake.

Alisema mara kadhaa viongozi wa serikali hiyo wamekuwa wakiwasiliana na serikali ya Tanzania kila wanapoona wavuvi haramu na ksiha vyombo vya usalama kwenda kuwakamata na kuwafikisha kunakohusika kwa hatua za kisherkia.

“Ni mara nyingi sana Sheli sheli imekua msaada mkubwa kwa Tanzania kwa sababu kule watu wamekuwa wakijaribu kuendesha uvuvi haramu lakini kila wakijaribu wanatupigia simu na serikali inachukua hatua haraka sana na imesaidia kwa kiasi kikubwa,” alisema

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Tumaini Gurumo alisema kwa mwaka chuo hicho kinazalisha mabaharia 100 ambao wanakidhi soko la ndani na wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba mbalimbali

“Soko la mabaharia ni kubwa sana sisi tunazalisha 100 kwa mwaka ambao wanakidhi mahitaji ya ndani na wengine wanakwenda kufanyakazi nje ya nchi, vijana wachangamkie fursa hii kwasababu inafedha za kutosha na ajira yake siyo ya kuhangaika,” alisema Dk. Tumaini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!