MGAHAWA kutoka Hong Kong uliofanya kazi takribani miaka 50 , umezama siku chache baada ya kuvutwa kutoka bandarini. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).
Jumba hilo lilitumbukia katika Bahari ya Kusini ya China wakati likielekea eneo lisilojulikana,kampuni mama inayomiliki mgahawa huo, Aberdeen Restaurant Enterprises imeripoti kuwa imehuzunishwa na tukio hilo sana , lakini wanashukuru hakuna wafanyakazi waliojeruhiwa.
Hata hivyo, mgahawa huo ulifungwa machi mwaka 2020 wakati wa janga la Covid 19 liliposhamiri.
Zaidi ya wageni milioni 3 wanaaminika kula vyakula katika hoteli hiyo, kwa miaka minginsana wakiwemo Malkia Elizabeth, Tom Cruise pamoja na Richard Branson.
Pia umeigiziwa filamu kadhaa ikiwa ni pamoja na filamu ya Bond, lakini janga la corona lilifanya biashara hiyo kuwa mbaya zaidi baada ya wageni kutotembeleapo tena.
Aidha meli hiyo ilipaswa kukaa katika eneo lisilojulikana huku ikisubiria mwendeshaji mpya.
Lakini ilizama siku ya jumapili tarehe19 juni 2022, karibu na Visiwa vya Paracel baada ya kukabiliana na hali mbaya , nakuanza kuingiza maji Aberdeen Rastaurant Enterpris ilisema.
Leave a comment