October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali imetumia Mil 400 kukarabati Kituo cha Afya Igoma

Kituo cha Afya Igoma, Mwanza

Spread the love

SERIKALI imeeleza, Kituo cha Afya Igoma kilipatiwa kiasi cha Sh. 400 milioni kwa ajili ya ukarabati na upanuzi na kazi hiyo imekamilika. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 15 Aprili 2020 bungeni na Wizara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakati ikijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Kemilembe Lwota (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua, ni lini serikali itapekeka vifaa tiba kama vile x -ray, Ultrasound na vifaa vingine vya kiuchunguzi kama ilivyoahidi.

“Serikali imefanya jitihada kubwa katika ujenzi na uboreshaji wa sekta ya afya kwa kujenga Vituo vya Afya kikiwemo kituo cha Afya Igoma. Je ni lini serikali itapekela vifaa tiba kama vile x -ray, Ultrasound na vifaa vingine vya kiuchunguzi kama ilivyoahidi?” amehoji Lwota.

Wizara imesema, Kituo cha Afya Igoma kilipatiwa kiasi cha Sh. 400 milioni kwa ajili ya ukarabati na upanuzi na kazi hiyo imekamilika

Aidha serikali imesema kuwa inaendelea kuvipatia vifaa tiba Vituo vya Afya vilivyokamilika ambapo hadi sasa jumla ya Shilingi bilioni 27.11 zimetumika.

“Kituo cha Afya Igoma kitapewa kipaumbele cha kupatiwa vifaa katika awamu zinazofuata ili kukiwezesha kutoa huduma” Serikali Imeeleza.

error: Content is protected !!