Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ugonjwa wa figo tishio Dar, Arusha
AfyaHabari za Siasa

Ugonjwa wa figo tishio Dar, Arusha

Figo ya binadamu
Spread the love

JIJI la Dar es Salamu linaongoza kwa kuwa na wagonjwa wa figo huku Arusha ikishika namba mbili. Mkoa wa Simuyu unaongoza kwa wagonjwa wachache Tanzania bara na Zanzibari. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 15 Aprili 2020, bungeni na Wizara ya Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati ikijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Mgeni Jadi Kadika (CUF).   

Mbunge huyo alitaka serikali ieleze, ni mkoa gani Tanzania Bara na Visiwani unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa figo.

“Ugonjwa wa figo unakuwa kwa kasi kubwa sana katika nchi yetu ya Tanzania, je, ni mkoa gani katika mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa figo?”amehoji mbunge huyo.

Wizara ya Afya ikijibu swali hilo, imeeleza ugonjwa wa figo husababishwa kwa kiasi kikubwa na magonjwa yasiyoambukiza.

Imesema, kulingana na utafiti ulioitwa “Community Base Survey to assess prevalence of kidney diseases mwaka 2013,” uliofanyika katika maeneo ya Kaskazini Mashariki ambayo ilihusisha Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Morogoro pamoja na Utafiti uliofanyika mwaka 2015, ulihusisha Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam ulionesha asilimia 44 unasababishwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu linachangia asilimia 34.

“Utafiti huo uliofanyika katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Morogoro mwaka 2013, ulionesha tatizo kuwa kubwa kwa asilimia 7 na takwimu za utafiti kwenye jamii uliofanyika Kisarawe na Dar es Salaam mwaka 2015, ulionesha tatizo kuwa kubwa kwa asilimia 12.4.

“Magonjwa yasioambukiza husababishwa na mtindo usio bora wa maisha ikiwa ni pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi, matumizi ya tumbaku na bidhaa zake, matumizi ya chumvi ya mezani, kutokufanya mazoezi na kwa ujumla na lishe mbaya, mfano matumizi ya mafuta kupita kiasi.”

Wizara hiyo imeeleza, viashiria vyote hivi huchangia kupata magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari, ambayo ndio husababisha zaidi ugonjwa wa figo.

“Tatizo hilo ni kubwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambako takwimu za kitabibu zinaonesha kuna wagonjwa 1,234. Mkoa wa pili kuwa na tatizo la wagonjwa wa figo wengi ni Arusha wenye idadi ya wagonjwa 563. Mkoa ambao una takwimu chache za wagonjwa wa figo ni Simiyu wagonjwa 113.

“Nitoe wito kwa wananchi kuendelea kufanya mazoezi kuepukana na magonjwa yasiyo ambukiza,” imeeleza wizara hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!