Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia akagua Hanang, awataka wananchi kuondoka maeneo hatarishi
Habari za SiasaTangulizi

Samia akagua Hanang, awataka wananchi kuondoka maeneo hatarishi

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi wa mji mdogo wa Katesh, wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara, waliokumbwa na maafa ya maporomoko ya udongo, kuondoka kwenye maeneo hatarishi ili wasipate madhara mengine. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi, ametoa wito huo leo tarehe 7 Disemba 2023, alipowasili mjini Katesh, kwa ajili ya kuwasalimia wahanga pamoja na kuangalia athari zilizosababishwa na maporomoko hayo yaliyotoka katika Mlima Hanang.

“Hili janga si letu pekee yetu mwaka jana lilitokea Malawi tumekwenda kuwasaidia, hatuwezi kujua Mungu anatuletea kwa kusudi gani ni kushukuru na kuchukua tahadhari sasa maeneo ya maji tuyapishe maji yachukue nafasi yake sisi tukae pembeni biashara iishe,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amewapa pole wananchi wa Hanang kwa athari walizopata kutokana na janga hilo, huku akiwaahidi kwamba Serikali iko pamoja nao na itahakikisha inawalinda.

“Poleni sana kwa tukio hili, huu msiba ni wa taifa wala sio wa wenu peke yenu. Marafiki zetu wanatoa pole sana, serikali tuko pamoja nanyi bado mawaziri, vikosi vya ulinzi na usalama na wengine wote wako hapa tunaangalia hali halisi jinsi ya kusaidia kuepusha wananchi kuingia tena kwenye balaa la aina hiyo,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika na maporomoko hiyo, pamoja na kwenda katika hospitali ya Mkoa wa Manyara, kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, alisema vikosi vya ulinzi vinaendelea kufanya shughuli za uopoaji miili ya marehemu, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi walioko katika maeneo yanayohofiwa kuwa hatarishi ili wahame mara moja.

“Wananchi wanatakiwa waondoke, El-Nino tuliyotabiri sasa ndiyo kipindi chake. Kwa hiyo kama mvua iliyonyesha kwenye hili tukio ilikuwa ndogo sana. Kuanzia kesho ni kutoa elimu watu waweze ondoka kwenye maeneo hatarishi,” alisema Mhagama.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, maporomoko hayo yaliyoambatana na mawe pamoja na miti mikubwa, yamebomoa nyumba katika baadhi ya maeneo.

Sendiga alisema shughuli za ukaguzi wa miili zinaendelea kufanywa, huku timu ya uokoaji ikiendelea kusafisha nyumba zilizochafuliwa na matope.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!