Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mitandao ya simu, Benki wapewa mbinu kupambana na ujangili
Habari Mchanganyiko

Mitandao ya simu, Benki wapewa mbinu kupambana na ujangili

Spread the love


WADAU wa maliasili wamekutana kujadili namna ya kudhibiti mianya ya upitishaji miamala ya fedha kwa njia mitindao na benki inayolenga kufadhili biashara ya maliasili na ujangili nchini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mjadala huo unaoratibiwa na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) iliwakutanisha wadau wa mitandao pamoja na benki ulioanza leo tarehe 7 na kutamatishwa kesho tarehe 8 Desemba 2023 jijini Dar es Saalam.

Godfrey Mondi Meneja Miradi wa TPSF amesema kuwa warsha hiyo ya siku mbili imelenga kutoa elimu kwa watoa huduma za kifedha kwa njia za benki na mitandao ya simu ili kudhibiti viashiria vya miamala ya fedha inayolengwa kufanyiwa biashara haramu ya kusafirisha Rasimali.

“Tunawajengea uwezo watu wa mitandao na benki ili kudhibiti miamala inayopita kwenye mitandao na benki inayoweza kuendesha biashara harama,” amesema Mondi.

Amesema kuwa mradi huo unaofadhiliwa na watu wa Marekani (USAID) unaitwa ‘Tuhifadhi Maliasili’ unalenga kupambana na ujangili.

Amesema kuwa miamala inayofanywa kwa kujirudia kwenye maeneo ya maliasili ni ya kuijengea shaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!