Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wazuiwa kutembelea waathirika maafa Hanang
Habari za SiasaTangulizi

Chadema wazuiwa kutembelea waathirika maafa Hanang

Spread the love

UJUMBE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), unaoongozwa na mwenyikiti wake Taifa, Freeman Mbowe, umedai kuzuiwa na Jeshi la Polisi kutembelea wahanga wa maporomoko ya udongo katika mji mdogo wa Katesh, wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hizo zimesambaa leo Alhamisi, katika mitandao ya kijamii, ambapo mmoja kati ya ujumbe huo ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbless Lema, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X, kuwa wamelazimika kukatisha safari yao kutokana na changamoto hiyo.

“Tumekatisha safari ya kuelekea Katesh- Hanang kuona wahanga wa mafuriko kutokana na vikwazo vingi tulivyokutana navyo, kuanzia tunaingia Manyara na zaidi vikwazo vikali tulipotaka kusalimia wagonjwa Hospital ya Rufaa Mkoa wa Manyara. Tunaendelea kuwapa pole sana wakazi wote Manyara. Tutaongea na vyombo vya habari kwa taarifa ya kina zaidi,” ameandika Lema.

Kada mwingine wa Chadema, Boniface Jacob, kupitia mtandao huo aliandika akidai tangu asubuhi, Mbowe na wenzake, wamezuiwa na Jeshi la Polisi mkoani Manyara, kutembelea eneo lolote lililokumbwa na maafa.

“Viongozi wa CHADEMA waliomba kwenda maeneo tofauti ambayo hayapo katika ratiba ya kutembelewa na Rais Samia, lakini pia Jeshi la polisi limekataa wasiende popote wala kuonana na majeruhi yoyote wilayani Hanang, pamoja na kukataliwa kupokelewa misaada yake kwa wahanga,” ameandika Jacob na kuongeza:

“Mwenyekiti alikuwa amebeba misaada mbalimbali ya  dawa za binadamu pamoja na vifaa vingine kwa ajili ya kuwagawia waathirika wa mafuriko hayo”

MwanaHALISI  imemtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani manyara, George Katabazi kupitia njia ya simu, ili kupata ukweli juu ya madai hayo, ambapo namba zake zilikuwa hazipatikani.

Tayari Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasili Katesh kwa ajili ya kuwapa pole wahanga wa janga hilo lililotokana na maporomoko ya sehemu ya miamba dhoofu ya Mlima Hanang, ambayo yalishindwa kuhimili mgandamizo kutokana na kunyonya maji.

Kaya zaidi ya 1,000 zimeripotiwa kuathirika na janga hilo lililosababisha vifo 69 na kujeruhi watu takribani 100.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!