Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia akabidhi boti 160 za uvuvi, vizimba vya kufugia samaki
Habari za Siasa

Samia akabidhi boti 160 za uvuvi, vizimba vya kufugia samaki

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka wizara ya mifugo na uvuvi kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kudhibiti na kutokomeza vitendo vya uvuvi haramu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza baada ya kuzindua na kukabidhi boti za uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kwa wavuvi wa kanda ya ziwa.

Boti za uvuvi

Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara hiyo kuwachukulia hatua kali za kisheria wavuvi wanaokiuka taratibu za uvuvi salamna.

Rais Samia pia amesema serikali inafanya jitihada kuinua sekta ya uvuvi nchini kwa kuimarisha utendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili iendane na dhamira ya mageuzi yaliyokusudiwa.

Vile vile, Rais Samia amesema kundi la vijana na wanawake linaongoza kushiriki kwenye ajira zisizo rasmi hivyo serikali inarasimisha shughuli zao kwa kuwawezesha kupata zana na nyenzo za kisasa ili kujikimu kiuchumi.

Vizimba vya kufugia samaki.

Rais Samia amesema serikali imejipanga kukuza sekta ya uvuvi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ununuzi wa meli za kisasa za uvuvi katika bahari kuu, ujenzi wa bandari za uvuvi katika maeneo ya Kilwa Masoko mkoani Lindi na Bagamoyo ili kuongeza pato la taifa.

Boti 160 za uvuvi wa kisasa zimezinduliwa kwa wanufaika 989 pamoja na vizimba 222 vinavyotarajiwa kugaiwa kwa wanufaika 1,213 katika mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu na Geita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!