Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Haya hapa majina ya madiwani 5 walioteuliwa na NEC
Habari za Siasa

Haya hapa majina ya madiwani 5 walioteuliwa na NEC

Ramadhan Kailima
Spread the love

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum watano kujaza nafasi wazi katika Halmashauri tano za Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Uteuzi huo uliofanyika katika kikao chake kilichofanyika jana Jumatatu, umetajwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura 292.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Mkurugenzi wa Uchaguzi,Ramadhan Kailima amesema uteuzi wa madiwani hao wanawake wa viti maalumu umefanyika baada ya tume kupokea barua kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.

Amesema waziri husika kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, aliitarifu tume juu ya uwepo wa nafasi wazi za madiwani wanawake wa viti maalum katika Halmashauri tano za Tanzania Bara.

Amesema nafasi hizo zimetokana na vifo vya Madiwani hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Tume baada ya kupokea taarifa hiyo ilimfahamisha Katibu Mkuu wa CCM juu ya uwepo wa nafasi wazi. chama hicho kiliwasilisha majina ya wanachama waliopendekezwa kuteuliwa kuwa madiwari wanawake wa viti maalum kama ifuatavyo;

“Mecha Goodluck Matile- Halmashauri ya Jiji la Tanga, Joyce Milembe Aenda- Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Sharifa Hassan Magalagala – Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Clementina Daudi Mateja Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa na Mariam Abdi Galu – Halmashauri ya Wilaya ya Chemba,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!