Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati: Isiwe lazima wakurugenzi kusimamia uchaguzi
Habari za SiasaTangulizi

Kamati: Isiwe lazima wakurugenzi kusimamia uchaguzi

Wapiga kura
Spread the love

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imependekeza kwamba sheria ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani isiweke ulazima kwa Mkurugenzi Mtendaji kusimamia uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kamati hiyo imependekeza kwamba badala yake, kuwepo na masharti ya mtumishi wa umma mwandamizi ama mtu mwingine yoyote mwenye sifa kuteuliwa kuwa msimamizi wa uchaguzi au msimamizi msaidizi wa Uchaguzi.

Akiwasilisha maoni ya kamati kuhusu muswada wa sheria ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2023 leo Jumanne bungeni jijini Dodoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Joseph Mhagama amesema Ibara ya 6(1) ya muswada huo inaeleza kuwa kila Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya atakuwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika Jimbo au Kata.

“Mheshimiwa Spika, Serikali iliona kuwa upo umuhimu wa Wakurugenzi Watendaji kutajwa kwenye sheria kwa kuwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya madai na. 138/2019 na Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu kwenye kesi ya madai na. 11/2020 ziliamua kuwa Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi haukiuki masharti ya Katiba wala Mkataba wa Afrika wa Watu na Haki za Binadamu mtawalia.

“Kamati bado ina maoni kuwa hakuna ulazima wa sheria kuweka sharti kwa Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi au wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa kuwa uzoefu unaonyesha wapo Wakurugenzi kwa sababu mbalimbali wanapoteza sifa za kuwa wasimamizi wa uchaguzi,” amesema.

Amesema kwa muktadha huo, Kamati imeandaa Jedwali la Marekebisho ya Kamati ya kuwatumia watumishi wa umma waandamizi ama mtu yoyote mwenye sifa kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika jimbo au kata.

Muswada huo uliwasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana na Januari mwaka huu, wadau mbalimbali walitoa maoni yao kuhusu muswada huo na miswada mingine miwili na sasa miswada hiyo imeanza kujadiliwa na wabunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!