May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samatta arudi tena Ubelgiji, aitosa Genk

Mbwana Samatta

Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amerejea tena katika Ligi kuu ya Ubelgiji baada ya jana tarehe 31 Agosti, 2021 kusajiliwa na klabu ya Royal Antwerp FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania amerudi Ubelgiji baada ya kupitia baadhi ya klabu ya Aston Villa ya Uingereza na Fenarbach ya Uturuki.

Samatta alishawahi kuitumikia KRC Genk ya Ubelgiji ambayo ilimuibua na kumfanya awike Ulaya kiasi cha kumpa faida ya kutua katika soka la England.

Mshambuliaji huyo baada ya kuondoka nchini Ubelgiji wengi walimtabiria mazuri lakini bahati haikuwa kwake katika sehemu alizopita hakupata nafasi ya kutosha kulinganisha na alipokua Ubelgiji katika klabu ya Genk.

Aidha, wengi walitarajia Samatta atarudi nyumbani katika klabu ya KRC Genk kama walivyofanya baadhi ya mastaa kurudi katika klabu zao za zamani.

Christiano Ronaldo amerejea Manchester united, Antonio Griezman amerejea Atletico madrid wakati Romelu Lukaku amerejea Chelsea.

error: Content is protected !!