Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la kina Mdee:Chadema yasema haitapeleka barua nyingine bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Sakata la kina Mdee:Chadema yasema haitapeleka barua nyingine bungeni

Spread the love

 

CHAMA cha Demokarsia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitapeleka barua nyingine kwenda kwenye uongozi wa Bunge, kulitaarifu msimamo wake wa kufukuza uanachama wabunge 19 wa viti maalumu, akiwemo Halima Mdee. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Msimamo huo umetolewa leo Jumatano, tarehe 9 Machi 2022, na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, alipulizwa suala hilo kupitia mtandao wa kijamii wa ClubHouse, akiwa nchini Ubelgiji.

Lissu amesema, Chadema hakitapeleka barua hiyo kwa kuwa ilishapeleka mara ya kwanza na uongozi wa mhimili huo ukakiri kuipokea.

“Ofisi ya Spika inayo taarifa ya maandishi ya uamuzi wa Chadema, ilipelekwa kwa Dispatch walisaini kupokea. Alipokea Spika Job Ndugai aliyekuwepo, alikubali kwamba ameipokea akasema yeye ndiye anayeamua. Kwa hiyo wana taarifa,” amesema Lissu.

Katika hatua nyingine, Lissu amesema hawana mpango wa kupeleka majina ya wabunge wengine, kama mbadala wa kina Mdee waliofukuzwa Chadema, kwa kuwa bado hawatambui matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yaliyozalisha nafasi hizo.

“Haya ni amswali ya watru wanaotaka tuhalalishe wizi wa uchaguzi, tuchukue ruzuku waseme eeeeh na Covid-19? kama mmechukua ruzuku kwa nini mnawakataa? Mkiwakubali Covid-19 watasema kwa hiyo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki?,” amesema Lissu.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

Lissu amesema kama Chadema kitawakubali wabunge hao, itakuwa nisawa na wamekubali uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki kitendo kitakachotafsiri kwamba kuna tume huru ya uchaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Lissu, baada ya Spika wa Bunge aliyejizulu hivi karibuni, Job Ndugai, kudai wabunge hao ni halali kwa kuwa Chadema hawakupeleka taarifa rasmi ya kufukuzwa kwao. Msimamo huo pia uliwekwa na Spika wa sasa, Dk. Tulia Ackson.
Mdee na wenzake walikata rufaa kupinga hatua ya kufukuzwa uanachama wa Chadema.

Mbali na Mdee, wengine waliokata rufaa kupinga kutimuliwa Chadema ni, waliokuwa viongozi wa Bawacha, Hawa Mwaifunga (Makamu Mwenyekiti). Grace Tendega (Katibu Mkuu). Jesca Kishoa (Naibu Katibu Mkuu) na Agnesta Lambart (Katibu Mwenezi).

Wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Ester Bulaya na Esther Matiko, pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mtwara, Tunza Malapo.

Halima Mdee

Pamoja na Cecilia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropita Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Wanasiasa hao walifukuzwa Chadema tarehe 27 Novemba 2020, siku mbili baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwa wabunge viti maalumu, tarehe 24 Novemba mwaka huo.

Wabunge hao walitimuliwa kwa kosa la usaliti, kufuatia hatua yao ya kukubali ubunge viti maalumu, kinyume na msimamo wa Chadema, wa kutopelekea wawakilishi bungeni wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Chadema kilipinga matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na wa haki. Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekanusha madai hayo ikisema ilisimamia uchaguzi kwa huo kwa mujibu wa sheria.

Katika matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na NEC, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilifanikiwa kushinda kiti cha urais pamoja na kuzoa viti vya ubunge zaidi ya 300, huku vyama vya upinzani vikiambulia viti sita vya ubunge wa jimbo na wabunge viti maalumu 19.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!