Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu asema mchakato katiba mpya mgumu, ataka safari ianze
Habari za Siasa

Lissu asema mchakato katiba mpya mgumu, ataka safari ianze

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Chadema Bara, Tundu Lissu, amesema mchakato wa upatikanaji katiba mpya ni mgumu, kwani unachukua muda mrefu na kushauri uanze mara moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 9 Machi 2022, akihutubia kupitia mtandao wa kijamii wa ClubHouse, akiwa nchini Ubelgiji.

Makamu Mwenyekiti huyo wa Chadema, amesema hata mchakato wa upatikanaji katiba mpya nchini Kenya, nao ulichukua muda mrefu, kwa kuwa ulianza 1998 hadi 2010, ilipoatikana.

“Kwa hiyo mchakato ni mgumu na kama mtu anaamini kwamba tunaweza tukaipata ndani ya mwaka mmoja Mungu amsaidie. Hatuwezi kuipata ndani ya mwaka mmoja, miwili, mitatu, minne au mitano.Lazima tuanze mchakato,” amesema Lissu.

Lissu amesema, muda wa kukamilika kwa mchakato huo utategemea na watu watakaoshiriki zoezi hilo.

“Urefu wa hiyo njia itaamriwa na hao watakaosafiri hiyo njia, tukisafiri kwa pamoja, kwa kukubalina na mambo ya msingi, njia itakuwa fupi. Tukiiafiri kwa kuvuta, kutoboana macho, kupigana na kufungana njia itakuwa ndefu zaidi,” amesema Lissu.

Mwanasiasa huyo amesema, kama mchakato wa upatikanaji katiba mpya hautakamilika ifikapo 2025, kuna uwezekano wa kufanya marekebisho madogo ya katiba kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu, huku ukiendelea.

Mchakato wa upatikanaji katiba mpya ulianza rasmi nchini Tanzania 2011, kwa utungwaji wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011, kisha ikatungwa Sheria ya Kura ya Maoni Na. 11/2013.

Mchakato huo uliendelea hadi 2015, ulipokwama katika hatua ya kura za maoni za kupitisha katiba pendekezwa, kutokana na zoezi la uandikishaji wapiga kura lililokuwa linafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutokamilika.

1 Comment

  • Asante ndugu lissu nakupongeza kwa kutimzmiza wajibu moja ya kazi ya kiongozi ni kuongea and kuonesha vitendo ambavyo wananchi wataviiga sasa lissu ukiwa kama kiongozi unawo waongoza waige nini kutoka kwa kwo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!