Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Michezo Sakata la idadi ya wachezaji wa kigeni laibuka bungeni
Michezo

Sakata la idadi ya wachezaji wa kigeni laibuka bungeni

Djuma Shaban akisaini mkataba wa kuitumikia Yanga
Spread the love

 

SERIKALI imesema licha ya kuwepo kwa idadi kubwa wa wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu Bara, itaendelea kulishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzingatia ushiriki wa wachezaji wa Kitanzania katika klabu mbalimbali za ligi hiyo ili watimize vigezo vya kuitwa katika timu ya Taifa. Anaripoti Erick Mbawala, TUDARCo … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka mjadala kuhusu ongezeko la idadi ya wachezaji 12 wa kigeni wanaoruhusiwa kusajiliwa na klabu vya Ligi Kuu tofauti na msimu uliopita ambao idadi ilikuwa wachezaji 10 pekee.

Hali hiyo imeelezwa kudumaza vipaji vya wachezaji wazawa ambao wanakosa vigezo vya kuitwa katika Timu ya Taifa.

Swali lililoulizwa leo tarehe 13 Septemba, 2022 bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba (CCM)  ambeya alitaka kufahamu ushiriki wa wachezaji wa ndani kwenye klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania.

“Moja kati ya kigezo cha wachezaji kuteuliwa katika timu ya Taifa ni kupata muda wa kutosha kucheza katika ligi za juu, yaani Ligi Kuu na ligi daraja la kwanza, je wachezaji wa ndani wanapata vipi nafasi,” aliuliza Tarimba ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SportiPesa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Michezo, Utamaduni na Sanaa, Paulina Gekuli amesema wataishauri TFF kuzingatia ushiriki wa vijana wa kitanzania licha ya idadi ya usajili wa kigeni waliyoitoa kupitia Baraza la Michezo la Tanzania (BMT) kuwa kubwa.

Amesema kwa mujibu wa Sheria, kanuni Namba 62 ya Wachezaji wa kigeni ya Ligi kuu, timu inauwezo wa kusajili wachezaji 12, wa kigeni na inaweza kuwachezesha wachezaji wote katika mechi ya ligi kuu au Ngao ya Jamii.

“Tunazingatia ushiriki wa vijana wetu katika Timu ya Taifa na tutaendelea kuishauri TFF, pamoja na kwamba wamesajili wachezaji kutoka nje kwa idadi maalum ambayo tumewapa kupitia BMT, wahakikishe vijana wetu wanapata nafasi waonyeshe vipaji vyao,” alisema Naibu Waziri huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!