Wednesday , 6 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Saa 48 za NEC kutatua uchukuaji fomu ubunge, udiwani
Habari za Siasa

Saa 48 za NEC kutatua uchukuaji fomu ubunge, udiwani

Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imeagiza vyama vya siasa vilivyokumbwa na changamoto za wagombea wao kunyimwa fomu za uteuzi, kuwasilisha majina kwa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo husika ndani ya siku mbili (sawa na saa 48). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Agizo hilo limetolewa jana Alhamisi tarehe 20 Agosti 2020 na Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, ambapo amevitaka vyama vilivyokumbwa na kadhia hiyo kupeleka majina ya wgaombea wake kuanzia jana hadi leo tarehe 21 Agosti 2020.

Agizo hilo la NEC limekuja baada ya vyama vya siasa vya upinzani ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo, kulalamika baadhi ya wagombea wao kunyimwa fomu za kugombea Ubunge na Udiwani kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

“Kutokana na changamoto hizo watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao wamejitokeza na kwenda kuchukua fomu za uteuzi za kugombea ubunge au udiwani na vyama vyao kushindwa kupatiwa fomu za uteuzi,” amesema Dk. Mahera.

Dk. Mahera ameongeza “Hivyo tume inatoa nafasi kwa vyama vya siasa kuwatambulisha wagombea wenu kwa wasimamizi wa uchaguzi, ndani ya siku mbili kuanzia tarehe ya barua hii wapewe fomu za uteuzi.”

“Hii ni kwa ajili ya majimbo na kata zilizo na changamoto au taarifa zake zimewasilishwa kwa tume,” amesema.

Majimbo ambayo wagombea wa Chadema walikuwa wamenyimwa fomu ni Kibamba, Kigamboni na Mabagala jijini Dar es Salaam pamoja na Kilombero mkoani Morogoro.

Nacho chama cha ACT-Wazalendo kimekutakana na changamoto hiyo katika Kata ya Upanga Magharibi. Changamoto hiyo imejitokeza baada ya wagombea wasioteuliwa na vyama husika, kuchukua fomu.

Akizungumzia changamoto hiyo, DK. Mahera amesema changamoto hizo zimetokana na vyama husika kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa wagombea wao kuchukua fomu.

“NEC  imefuatilia zoezi la kuchukua fomu za uteuzi na kubaini kuna changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na vyama vya siasa kutojipanga na kuweka utaratibu mzuri wa wagombea wao kuchukua fomu za uteuzi,” amesema Dk. Mahera.

Zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu linatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 25 Agosti 2020 na kisha siku hiyo hiyo uteuzi wa wagombea katika uchaguzi huo unafanyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!